Na Woinde Shizza, ARUSHA
SERIKALI pamoja na sekta binafsi zimetakiwa kukaa pamoja ili kubuni mikakati ya namna ya kuendesha sekta muhimu za uchumi kama vile sekta ya utalii, sekta ya usafirishaji, sekta ya kilimo, sekta ya nishati pamoja na ufugaji bila kungoja kuisha kwa janga la Corona 19.
Hayo yamebainishwa na Mtendaji mkuu wa marafiki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Moses Adam wakati akizungumza na mwandishi wetu ambapo alisema wanatakiwa kuja na njia mbadala endelevu zitakazoendelea kuendesha izo sekta ili ziweze kuwa vizuri na kukuza uchumi.
Alisema kuwa ni jambo la muhimu sana sekta binafsi pamoja na seikali kukaa na kuangalia njia sahihi zitakazo weza kunusuru uchumi wetu, kwa kukutana kwa pamoja na kujadili njia sahihi zitakazo saidia kunusuru uchumi wetu, pamoja na kusaidia biashara na kazi kuendelea kama zamani bila kusubiri ugonjwa huu wa Corona 19 kuisha kwani haijulikani utachukuwa muda gani hadi kumalizika .
Alisema wakianzia na sekta ya utalii inaweza kuendelea pamoja na janga hili kuwepo wanaweza wakachukuwa watalii kwa njia maalumu ambayo haitawaathiri wala haita wakutanisha na watu, ambapo alibainisha njia moja wapo ni kuwachukuwa moja kwa moja kutoka wanapo tua katika kiwanja cha ndege na kuwapeleka moja moja katika hifadhi zetu kuangalia vivutio.
“kwa mfano wanaposhuka katika uwanja wa ndege wakichukuliwa na kampuni husika ambayo walikuwa tayari wamewasiliana nayo katika hali ya taadhari ile ile inayotakiwa kujikinga na ugonjwa wa Corona na pia inawezekana kabisa kukawa na vipimo kabisa tofauti na upimaji joto, serikali inaweza ikaamua kuweka gharama za upimaji katika ratiba kamili ya utalii wao (pakeji ya gharama ziwe ndani ya gharama zote za utalii) na mtalii ajulishwe kabisa atakapo kuja Tanzania aambiwe kabisa ataletwa na kwenda kupimwa kabisa majibu yatakapo patikana ndio aruhusiwe kwend ambugani na kama akigundulika anaugonjwa basi awekwe kizuizini (karantini) kwa gharama zake au arudishwe kwao “alisema Mosses
Alisisitiza iwapo sekta hizi zitakaa na kupata majibu ya namna ya kufanya basi majibu yale yapelekwe katika kila sekta, na kwa upande wa sekta ya utalii matangazo yarushwe ili wageni waliopo nje wakiona matangazo haya wajue kabisa wakija hapa nchini wanatakiwa kufanya nini nani.
Alibainisha pia wafanyakazi wa sekta hizo wanatakiwa waandaliwe na wapewe elimu ya namna ya kujilinda dhidi ya maambukizi na namna ya kuwahudumia wageni hawa wanaokuja katika kipindi hichi cha ugonjwa huu wa Corona 19 na ikiwezekana kuwe na kambi maalumu kwa ajili ya kuwaweka wafanyakazi wote wakiwemo waongoza watalii ambao wanawahudumia wageni wote wanaotembelea vivutio vyetu pamoja na sehemu mbalimbali hadi pale ugonjwa huu utakapo bainika umeisha kabisa .
“Tunaitaji kuendelea kuingiza kipato na kukuza uchumi wan chi yetu hivyo ni vyema shughuli zetu za kukuza uchumi kuendelea kufanyika kama kawaidia, tukiendelea kukaa na kubweteka bila kuangalia namna ya kufanya basi tutazidi kudidimiza uchumi wetu na hata tukiangalia sasa hivi hali imeshakuwa mbaya tangu ugonjwa huu uingie, kwani makampuni mengi ya utalii yameshafugwa, hotel zimefungwa, viwanda vimefungwa na vijana wengi wamekosa ajira sasa serikali pamoja na sekta zetu binafsi tusipo fanya jambo mapema tutapata shida san asana”alibainisha Mosses
Alisema kuwa wadau wa sekta binafsi pamoja na serikali wanatakiwa kuanza kujipanga katika kutafuta masoko ya nje na yandani, na kwa upande wa masoko ya ndani waanze kuhamasisha watu kufanya kazi na katika sekta ya utalii ambayo ndio imeharibiwa sana na imesimama kwa sasa ni vyema kuangalia ni namna gani au ni kitu gani kitafanyaka ili sekta hii iendelee kufanya kazi kwani asilimia kubwa ya uchumi wetu inategemea sekta hii kwani asilimia kama 17% ya pato la taifa inatokana na utalii.
Alisema kwa upande wa sekta ya usafiri wa anga wanaweza wakaamua kufunguwa anga lakini wakaamua kuweka sharia ya kuendelea kupima wageni kabla ya kutoka kwao na wanapoingia wakifika katika viwanja vyetu vya ndege wapimwe, na wale ambao wanapitia mipakana nao wapimwe wahakikiwe ndio waruhusiwe ku ingia nchini.
Aliwahamasisha watanzania kuendelea kufanya kazi kwa bidii kama vile Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli anavyoendelea kusisitiza kufanya kazi bila woga wala kujibweteka, huku akiwasihi waendelee kuchukuwa taadhari ambazo wizara ya afya inazitoa kila kukicha.
No comments:
Post a Comment