Serikali ya Tanzania inatumia Sh7 bilioni kujenga kituo maalumu cha kuhudumia wagonjwa wa corona katika eneo la Kisopwa ambalo lipo kilometa moja kutoka hospitali ya Mloganzila.
Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imeeleza kuwa kituo hicho ambacho kinajengwa upesi kitawekewa miundombinu ya kisasa kurahisisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa virusi hivyo.
Pindi kitakapokamilika kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa 200 kwa pamoja.
Mradi huo unatekelezwa na Jeshi la kujenga Taifa kupitia kampuni yake ya Suma JKT na tayari askari 389 wamepelekwa eneo la mradi.
No comments:
Post a Comment