KANISA la ANGLIKANA latoa SEMINA kwa WALIMU wa SHULE zake zote kuhusu VIFAA vya KUJIKINGA na CORONA! - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, June 26, 2020

KANISA la ANGLIKANA latoa SEMINA kwa WALIMU wa SHULE zake zote kuhusu VIFAA vya KUJIKINGA na CORONA!





Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Kuelekea kufunguliwa kwa shule zote na shughuri mbalimbali hapa nchini, Kanisa la Anglikana Dayosisi ya kati Dodoma, imetoa semina kwa walimu wakuu na wasaidizi katika shule zote zinazomilikiwa na kanisa hilo sambamba na ugawaji wa vifaa vya kujikinga na Corona vyenye thamani ya shilingi milioni therathini na nne mil.34.

Akizungumza wakati wa kufunga semina hiyo jijini Dodoma sambamba na zoezi la kugawa vifaa hivyo kwa shule zote zilizochini ya kanisa hilo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi amesema kanisa hilo lilikuwa msaada mkubwa katika mapambano dhidi ya corona.

"Baba askofu nasema kanisa hili limekuwa msaada mkubwa katika mapambano hayo na mmetoa vifaa vingi mmesaidia sana hata kwa maombi pia mpaka Corona tunakaribia kuimaliza kabisa hapa nchini"

"Mtakumbuka wakati wa kutangaza kufungua shule Rais alisema ugonjwa umepungua sio umeisha nafurahi ninyi mmetoa vifaa hivi kwa ajili ya kukabiliana na corona ili wanafunzi wawe salama kwa hilo nawapongeza" amesema DC Katambi.

Amelipongeza kanisa hilo kwa zoezi la kuanzisha shule katika maeneo mbalimbali hasa kwa shule ya watu wenye mahitaji maalumu ya Bwigiri kwani imekuwa msaada mkubwa kwa watu wenye ulemavu wa kuona na ngozi waliokuwa wamekosa matumaini.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya kati Dodoma Dkt Dickson Chilongani, amesema mpaka Sasa wanamiliki shule saba (7) na vyuo vitatu kwa upande wa shule inawanafunzi elfu mbili na ishirini (2020) na wote watapata barakoa wanapoanza masoma.

Ametaja vifaa walivyovitoa kuwa ni ndoo za kunawia na sabuni, vitakasa mikono, na vifaa vya kupimia joto la mwili na kila shule itapata vipima joto viwili ili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa salama wawapo shuleni.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages