MATOKEO ya AWALI uchaguzi URAIS Malawi UPINZANI waongoza! - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, June 26, 2020

MATOKEO ya AWALI uchaguzi URAIS Malawi UPINZANI waongoza!


Chombo cha habari cha Serikali nchini Malawi kimeripoti kuwa upinzani unaelekea kupata ushindi katika kura ya uchaguzi wa Urais unayofanyiwa marudio baada ya matokeo yake kufutiliwa mbali kufuatia madai mengi ya udanganyifu. 

Matokeo rasmi ya uchaguzi wa Urais Nchini Malawi uliofanyika siku ya Jumanne hayajatangazwa na tume ya uchaguzi ya Malawi. 

lakini chombo cha habari cha serikali MBC kinasema kwamba kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera anaongoza na asilimia 59 ya kura zilizohesabiwa.

Rais Peter Mutharika , ambaye anawania muhula wa pili ana asilimia 38 ya kura zilizohesabiwa, kinasema. 

Mgombea wa tatu ambaye hakuonekana kama mgombea mkuu Peter Kuwani anasemekana kujiapatia asilimia 2 ya kura hizo.

Mwaka uliopita, Malawi ilikuwa nchi ya pili barani Afrika kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais kufuatia madai ya udanganyifu, baada ya Kenya 2017. 

Mahakama iliingilia kati na kubadilisha matokeo katika eneo ambalo wizi wa kura ni suala la nyeti.

Wafuasi wa bwana Chakwera tayari wameanza kusherehekea kile wanachoamini ni ushindi wa kihistoria - katika kile kinachoaminika kuwa tukio la kwanza katika eneo la sahara kwamba uchaguzi uliokumbwa na udanganyifu umebadilishwa na upinzani kuibuka na ushindi ukichukua madaraka kwa njia ya kidemokrasia.

Pongezi pia zimetolewa na viongozi wa upinzani katika mataifa ya Afrika ya kusini.

"Maisha mapya kwa Malawi!," alisema kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa. 

"Mungu ameipatia Malawi Mcha Mungu'', aliongezea akitaja historia ya Chakwera kama kiongozi wa dini.

''Ndugu yangu, rafiki yangu na kiongozi ameshinda uchaguzi wa Malawi. Niliwasiliana naye kwa simu na kusherehekea ushindi wake'', alituma ujumbe wa twitter kiongozi wa zamani wa chama cha upinzani cha DA Mmusi Maimane.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages