MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia Chama hicho Yosepher Komba akizungumza na washiriki wa semina maalumu kwa wasichana mkoani Tanga iliyoandaliwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Wanawake na Uongozi yenye makao makuu yake Jijini Dar es Saalam.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini na Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia Chama hicho Yosepher Komba akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke na Uongozi Shamira Mshangama.
Sehemu ya washiriki kwenye semina hiyo
Sehemu ya washiriki kwenye semina hiyo
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia Chama hicho Yosepher Komba kushoto akimpongeza mmoja wa washiriki katika semina hiyo ambaye alitoa utenzi wake.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia Chama hicho Yosepher Komba kushoto akifurahi jambo na washiriki wa semina hiyo.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia Chama hicho Yosepher Komba na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke na Uongozi Shamira Mshangama wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia Chama hicho Yosepher Komba na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke na Uongozi Shamira Mshangama wakiwa kwenye picha ya pamoja.
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba amewapa mbinu wanawake wanaotaka kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwezi Octoba mwaka huu hapa nchini ili kuweza kushinda kwenye maeneo yao.
Ametoa mbinu hizo wakati akizungumza katika semina maalumu iliyoandaliwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Wanawake na Uongozi yenye makao makuu yake Jijini Dar es Saalam ambapo alisema upo umuhimu wao kuzingatia hayo iwapo wana dhamira ya dhati kutaka kugombea nafasi za uongozi.
Semina hiyo ilishirikisha wajumbe wanawake kutoka vyama vitano vyenye uwakilishi ambavyo ni Chadema, CCM, NCCR Mageuzi, ACT na Chama cha Wananchi CUF ambapo aliwausia wajumbe hao kutambua kuwa kampeni za uchaguzi sio rahisi na wanavyofikiria.
Yosepher ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini alizitaja mbinu hizo ni rasilimali watu, muda, fedha na taarifa ya eneo husika vitu ambavyo vikizingatiwa na mgombea yoyote anaweza kupata mafanikio katika harakati zake za kisiasa.
“Ndugu zangu hizo ni mbinu muhimu sana hasa unapotaka kusaka uongozi wa kisiasa hivyo tambueni rasilimali watu mnapaswa kulipa kipaumbele sana kwani ndio silaha ya ushindi na kuweza kuwafikisha kwenye mahali mnapotaka”Alisema Makamu Mwenyekiti huyo.
Aidha aliwataka wanasiasa wanawake mkoani Tanga kujiamini na kuchukua hatua pindi wanapojitokeza kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kufanikisha ndoto zao wa kuwatumikia wananchi katika maeneo mbalimbali.
Awali akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke na Uongozi Shamira Mshangama alisema katika mafunzo ya siku mbili yalikuwa yamejikita kuhamasisha wasichana walio ndani ya vyama vya siasa kuweza kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Alisema mafunzo hayo yameshirikisha vyama vitano ambapo kila kimoja kimetoa wajumbe sita walikuwa na utayari wa kutia nia ya kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao ikiwemo ubunge na udiwani ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko kwenye jamii.
Mkurugenzi huo alisema kwamba mradi huo wa “Nakataa Vikwazo Nagombea” unaendeshwa na Shirika la Mwanamke na Uongozi ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Voice .
No comments:
Post a Comment