CHANZO CHA PICHA,
AFP
Maelezo ya picha,
Pierre Nkurunziza alipokuwa akimfanyia kampeini mgombea wa urais wa chama tawala mwezi uliyopita
Pierre Nkurunziza,ambaye alizua hali ya sintofahamu baada ya kuwania uchaguzi wa rais kwa awamu ya tatu, alikuwa kiongozi wa Burundi kwa miaka 10 tayari.
Mwaka 2015, rais huyo aliyeingia madarakani baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha mauaji ya watu 300,000 , alisema kuwa hatawania tena ,nafasi hiyo ya urais kwa sababu ni kinyume na katiba.
Wafuasi wake walitetea kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2005 alichaguliwa na bunge na si wapiga kura- na kutetea hoja hiyo katika mahakama ya katiba ya nchini humo.
Na kiongozi wa zamani wa waasi alijisifu kuwa ameleta amani katika utawala wake nchini Burundi.
Iliripotiwa kuwa maasifa wa diplomasia walifika kuzungumza na bwana Nkurunziza ambaye alikuwa nje kidogo ya mji mkuu , Bujumbura, walimkuta rais huyo akiwa analima na wanakijiji.
CHANZO CHA PICHA,
AFP
Alikuwa anapanda miti ya parachichi ambayo warundi wengi huwa wanaiita miti hiyo jina lake "amaPeter".
"Mfumo wake wa maisha ya kawaida , amekuwa akiwavutia watu wengi wa vijijini kwa sababu ya muda mwingi ambao amekuwa akitumia kukaa nao kijijini, iliandikwa katika mtandao wa serikali wa Burundi.
Kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, Nkurunziza ambaye alihitimu masomo ya michezo alikua mkufunzi msaidizi katika chuo kikuu Cha Burundi.
Nkurunziza alikua muumini wa dhati wa dini ya kikristo ( Mlokole) . Alikua pia kocha wa timu ya daraja la kwanza mwanzoni mwa miaka ya 1990 . Na baadae kumiliki timu ya hallelujah ambayo pia alikua akishiriki kucheza mpira katika nafasi ya ushambuliaji na alikuwa akifunga mara kwa mara.
Chapisho la wasifu wake linasema kuwa jina la timu hiyo linaonesha wazi imani yake ya dini ya kikristo.
CHANZO CHA PICHA,
AFP
Baba yake ambaye alikua gavana, aliuawa katika mauaji ya halaiki ya wahutu mwaka 1972. Baba yake alikua mkatoliki na mama yake ni madhehebu ya anglikana.
Alikua hawezi kusafiri bila timu yake ya mpira pamoja na kikundi cha kwaya.
Yeye na mke wake waliwahi kuripotiwa kuwaosha miguu watu waliokuwepo kwenye mkusanyiko.
Yeye na mke wake Denise waliwahi kuripotiwa kuwaosha miguu watu waliokuwepo kwenye mkusanyiko.
Sio tu watu ambao Nkurunziza alikua na imani kuwa wanamuamini. Bali uongozi wake pia aliamini ni kutoka kwa Mungu.
"Ana amini kuwa ni kiongozi kwa matakwa ya Mungu, na hivyo anashughulika na serikali yake katika matakwa hayo" alisema msemaji wake Willy Nyamitwe.
Wakosoaji wake ikiwemo wapinzani kutoka vyama karibu 40 na watetezi wa haki za binadamu, wao wana mtazamo tofauti kumhusu.
Wanamtuhumu kuwa dikteta na ambaye hataki kuachia madaraka kutokana na kuongoza kwake kwa mihula mitatu.
CHANZO CHA PICHA,
AFP
Idadi kubwa ya watu waliuawa katika maandamano ya kumpinga kugombea muhula wa tatu. Wengine zaidi ya 100,000 walikimbia makazi yao kwenda nchi jirani kuhofia usalama wao na kwa hofu kuwa nchi hiyo ingetumbukia kwenye mzozo kwa mara nyingine
Lilifanyika jaribio la kumpindua ambalo halikufanikiwa.
Mkuu wa zamani wa majeshi Godefroid Niyombare aliongoza mpango huo wa kutaka kumuondoa madarakani mwaka 2015. Baada ya kushindwa kwa mpango huo wapinzani wakadai kuwa uchaguzi wa mwaka huo haukua wa uhuru wala haki.
Mkuu wa kitengo cha haki za binadamu cha Umoja wa mataifa bwana Zeid Raad al-Hussein alitoa wasiwasi wake kuhusu kundi moja la vijana la imbonerakure washirika wa Nkurunziza.
Kilishukiwa kufanya mauaji , kuwatesa watu na kuwapiga na kimekuwa hali kuwa mbaya nchini humo kwa muda," alisema.
Kikundi cha waasi cha wahutu cha CNDD-FDD kilichoongozwa na bwana Nkurunziza wakati wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na kusababisha kifo cha rais wa kabila la wahutu bwana Melchoir Ndadaye mwaka 1993 - alikuwa anahusika katika matukio kadhaa.
CHANZO CHA PICHA,
REUTERS
Ikiwemo kutekeleza vitendo kadhaa vya uvamizi katika barabara kuu za nchini humo, kuwaua wasafiri wengi, wakiwemo watu wa kabila la Tutsi
Alinyanyua silaha ili kupambana kukomesha utawala ulioongozwa na jamii ya kabila la waliokuwa wacheche Tutsi.
Nkurunziza alihukumiwa kifo na mahakama ya Burundi bila yeye kuwapo mahakamani mwaka 1998 kwa kosa la kutega mabomu ya ardhini, lakini alipata msamaha chini ya makubaliano ya amani yeliyokuwa na nia ya kumaliza mapigano.
Mwaka 2014 alijaribu na kushindwa kubadili katiba, ambayo inatoa ukomo wa madaraka kwa chama chake cha CNDD-FDD kwa kutoa hakikisho kwa makundi ya jamii ya watutsi kuwapatia nafasi mbalimbali katika taasisi za kiserikali.
Alikosolewa na umma kuwa anataka kusababisha vita nyingine ya kikabila.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment