Ajali yatokea Mlandizi magari manne yagongana, Wananchi watakiwa kutumia barabara ya Bagamoyo - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, July 2, 2020

Ajali yatokea Mlandizi magari manne yagongana, Wananchi watakiwa kutumia barabara ya Bagamoyo


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, amewataka watumiaji wa barabara ya Morogoro kutumia njia ya  barabara ya msata baada ya kutokea ajali ya magari manne katika daraja la Mkalamo Mlandizi.

Ajali hiyo imetokea  usiku wa kuamkia  leo Julai 02,2020 imesababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi watatu.

Tukio hilo limesababisha kuwepo kwa foleni kubwa na  polisi kuifunga barabara hiyo kwa muda kutokana na ajali hiyo.

Kamanda Nyigesa amesema Jeshi la polisi mkoani Pwani linaendelea na jitihada za kutoa magari hayo yaliyofunga njia.

Habari za awali inadaiwa kuwa lori la mafuta limegongana na gari jingine na kusababisha magari mawili kugongana katika eneo hilo.

Habari hii itaendelea..

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages