Thursday, July 2, 2020

Zantel Yazindua Duka Jipya lililopo Vuga, Wazingatia Afya za Wateja Wao
Wateja wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel wakipata huduma katika Duka jipya la Zantel la Vuga baada ya kuboresha na kufanyiwa matengenezo makubwa ili kutowa huduma bora kwa wateja wao. na kuzingatia ushauri wa Wataalam wa Afya.
Mfanyakazi wa Duka la Zantel Vuga Jijini Zanzibar akitowa huduma kwa mtaji wa kampuni hiyo alipofika kupata huduma hiyo.
Zanzibar. Wateja wa Zantel waliopo Zanzibar sasa watafurahia kupata huduma za mawasiliano zilizoboreshwa zaidi katika duka jipya la Zantel lililopoVuga Jijini baada ya kufanyika kwa maboresho ili kukidhi mahitaji ya wateja.
Duka hilo la kisasa limezingatia pia afya za wateja kwa kuwekewa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona (Covid-19) ikiwamo sehemu maalumu za kuoshea mikono pamoja na ukaaji foleni wa kuzingatia umbali wa mita mbili.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Zantel - Zanzibar.Ndg. Mohamed Khamis Mussa Baucha alisema duka hilo lenye zaidi ya miaka 20 limeboreshwa kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia ili kukidhi mahitaji ya huduma kwa wateja wake.
“Hili duka tumelifanyia ukarabati wa hali ya juu ili liwe imara na tumeliimarisha katika nyanja zote. Sisi mara zote tunasikiliza kero za wateja wetu na moja ya kero ilikuwa ni foleni hivyo tumeleta mfumo maalumu wa kukaa kwenye foleni (Queuing system) ambao utapunguza msongamano,” alisema.
Mfumo huo unaruhusu mteja kujisajili kwenye mtambo maalum na kupewa namba atakayoitumia wakati anasubiri huduma kwenye foleni na ataitwa mara tu zamu yake itakapofika hali inayofanya kuwa na ufanisi wa huduma.
Vile vile, duka hilo linauwezo wa kutoa huduma kwa wateja zaidi ya 100 kwa siku na kwamba kwa maboresho hayo wataweza kuhudumia wateja wengi zaidi kwa haraka zaidi.
“Nategemea tutahudumia wateja wengi zaidi kwa haraka kwa hiyo nawakaribisha wateja waje wajionee duka jipya na la kisasa ambalo ni duka la kwanza la Zantel Unguja,” alisema Meneja wa Maduka ya Zantel Zanzibar.Bi. Mwajuma Senkanga.
Huduma zinazopatikana dukani hapo ni pamoja na huduma ya Ezypesa, kusajili namba za simu, pamoja na bidhaa za mawasiliano kama vile simu.
Tags
# BIASHARA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
Ajali yatokea Mlandizi magari manne yagongana, Wananchi watakiwa kutumia barabara ya Bagamoyo
Older Article
GWAJIMA kugombea UBUNGE - KAWE kwa tiketi ya CCM!
Absa Group Reports 10% Increase in 2024 Earnings after Material Second-Half Recovery
Hassani MakeroMar 11, 2025Benki ya NBC Yaandaa Hafla ya Futari Zanzibar, Yajivunia Ongezeko la Wateja
Hassani MakeroMar 07, 2025BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA RASHAL ENERGIES, INAYOJENGA BOMBA LA GESI KISEMVULE-MBAGALA
Hassani MakeroMar 07, 2025
Labels:
BIASHARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment