GWAJIMA kugombea UBUNGE - KAWE kwa tiketi ya CCM! - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, July 2, 2020

GWAJIMA kugombea UBUNGE - KAWE kwa tiketi ya CCM!


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima, ametangaza nia ya kutaka kugombea ubunge katika jimbo la kawe.

Gwajima ametoa uamuzi huo jana kwamba atagombea kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo.

Jimbo hilo ambalo linashikiliwa na aliyekuwa mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.

Gwajima jana alifika katika ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kuchukua fomu na kupokelewa na viongozi wa chama hicho.

“Mimi nilikwenda pale kama mimi kama mlivyomsikia mheshimiwa Rais na  Dk Bashiru alivyosema wale watu wenye nia ya kumsaidia mheshimiwa Rais kuwatimizia wananchi adhima yao basi waanze kupitapita kwenye ofisi za chama na kuangalia nini kinawezekana,’ alisema Gwajima.

Aliongezea kuwa “Na mimi nikaanza kupita pita pale kuangalia na nimuombe na Mungu nione kama Mungu akiniruhusu nitaendelea. Nimefika pale nimemkuta Mwenyekiti na Katibu wakanipa maelekezo na miiko ya kufanya,” alisema Gwajima.

Alisema yeye anaishi Kawe “Nitagombea Kawe naona kunanoga pako vizuri,”

Juzi Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ally Bashiru alitangaza wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali ruksa kuanza kujitokeza na kuchukua fomu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages