Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dr. Bernard Kibesse. |
Benki ya I&M imezindua tawi lake kuu jijini Dar es Salaam na kuzindua akaunti maalum kwa wanawake ikiwa na lengo la kutoa nafasi kwa Watanzania kupata huduma za kibenki katika mazingira yanayoendana sambamba na kutangazwa kwa nchi kuwa ya uchumi wa kati.
Matukio haya makubwa mawili yamefanyika siku ya Jumatano 15 Julai 2020.
Tawi hili jipya ni ushahidi tosha kama nadhiri ambayo benki iliweka kwa ajili ya kuhudumia soko na wateja wake ambapo imekuwepo kwa takribani kwa ujumla, kwa kipindi cha miaka kumi tangu ilivyochukua benkin ya CF Union mwaka 2010.
Dr Bernard Kibesse, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, aliezindua tawi hilo aliendelea kwa kuipongeza benki hiyo kwa msaada mkubwa inayotoa kwenye maendeleo ya kiuchumi kwa taifa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dr. Kibesse aliisifu benki ya I&M kwa kuelewa mahitaji ya wateja wake na kuhakikisha imetimizia mahitaji hayo kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya kupatia huduma wanapotembelea matawi ya benki hiyo, “kuwepo sokoni kwa muda wa miaka kumi kumi mkikua mkikitengeneza faida, huku mkiendelea kuwahakikishia watanzania huduma bora sio jambo dogo, hivyo naipongeza benki ya I&M na uongozi wake kwa ujumla kwa jitihada hizi chanya.
Benki ya I&M imetumia fursa ya hafla hiyo kuitambulisha sokoni huduma yake mpya ya akaunti ya Tunaweza ambayo ni maalum kwaajili ya wanawake kwa ngazi ya mtu mmoja mmjoja, wajasiriamali hadi vikundi au taasisi, alisema Balozi mstaafu Bertha E. Semi-Somi, ambaye ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa benki ya I&M, ambaye naye alikuwepo kwenye hafla hiyo na kuizindua akaunti hiyo mpya ya wanawake, alisema akaunti hii maalumu ni kama chachu ya kuwaletea maendeleo wanawake, kuwajengea tabia ya kujiwekea akiba na kutimiza mahitaji yao na y a kifamilia kwani mama ndio nguzo ya familia kwenye jamii. Aslisema akaunti hii ina sifa za kipekee kama vile kutokua na makato ya mwezi wala makato ya kuweka fedha wakati mteja anapotoa pesa ambapo inawapa fursa wakina mama hasa wale walio kwenye vikundi wanaopata changamoto ya kuweka pesa zao sehemu salama.
Nimefurahishwa sana kwa mgeni rasmi kuitikia wito na kukubali kuja kuzindua tawi letu hili, na kushuhudia uzinduzi wa akaunti yetu ya wanawake ya Tunaweza ambayo imeonekana kukubalika Zaidi sokoni. Miaka hii kumi ya uwepo wetu kwenye soko, tunawahakikishia watanzania huduma bora kwani benki yetu ni moja ya benki zinazotoka kwenye kampuni kubwa Afrika mashariki, ijulikanayo kama I&M Holdings iliyopo Kenya. Alisema Bw. Baseer Mohammed, Afisa mtendaji mkuu wa benki ya I&M.
“Tunawapongeza sana waanawake kwa kuwa na moyo wa kujituma na kusimamia familia
kwenye jamii zetu. Hivyo tunaamini wajibu wetu kama taasisi kuhakikisha tunatoa fursa kwa wanawake kuwekeza kwaajili ya maendeleo yao na jamii nzima. Akaunti hii maalum tuliozindua leo ina sifa za kipekee kabisa kwani ni ya gharama nafuu katika kufanya miamala na haina makato ya mwezi wala makato wakati wanapotoa, hii inawapa fursa wanawake katika nyanja mbalimbali.
Benki ya I&M inayo matawi katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Moshi.
No comments:
Post a Comment