Kifo cha mwanafunzi katika sufuria ya chai chaibua mapya Dar - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, July 23, 2020

Kifo cha mwanafunzi katika sufuria ya chai chaibua mapya Dar


Na Gloria Tesha, Dar es Salaam

Kifo cha mwanafunzi wa darasa la kwanza kwa kusukumwa na wenzake kwenye sufuria ya chai ya moto kimeibua wazazi na kuipa neno Serikali.

Mwanafunzi Nanzia Samwel (6) aliyekuwa akisoma darasa la kwanza katika Shule ya St Anne Marie, Mbezi kwa Msuguli jijini Dar es Salaam, alikumbwa na mauti baada ya kusukumwa na wenzake na kuanguka ndani ya sufuria iliyokuwa na chai ya moto.

Kutokana na tukio hilo, wazazi wa marehemu wamehimiza Serikali kusimamia miundombinu ya shule zote nchini ili kuhakikisha inakuwa rafiki kwa wanafunzi na hivyo kuepusha majanga yanayogharimu maisha ya watoto.

Kwa mujibu wa mama mkubwa wa marehemu Happiness Mtenga, uongozi wa shule hiyo uliieleza familia hiyo kuwa, mtoto wao alisukumwa kwa bahati mbaya na mwenzake wakiwa kwenye foleni ya kuchotewa chai na kutumbukia kwenye sufuria lililokuwa na chai ya moto.

"Tunaiomba Serikali ifanye ukaguzi katika shule zote nchini, hii itasaidia kuhakikisha kunakuwa na usimamizi mzuri kwa watoto lakini pia miundombinu mizuri isiyohatarisha maisha ya watoto au mtu mwingine yeyote," alisema Mtenga aliyeeleza pia kuwa marehemu anazikwa leo saa tisa alasiri katika makaburi ya Mbezi Kibanda cha Mkaa, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages