OCHA/Steve
Hafez | Mjane akiwa na mjukuu
wake katika kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Mkoa wa Idleb,Syria.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameuambia ulimwengu
wa nchi za Kiarabu kwamba sasa ni wakati wa kugeuza janga la virusi vya Corona
au COVID-19 kuwa fursa ya kujijenga upya na kwa ubora zaidi.
Guterres
kupitia taarifa ya kisera kuhusu janga la COVID-19 na jinsi ya kujikwamua vyema katika nchi za
ulimwengu aliyoitoa hii leo amesema janga hilo limedhihirisha mapungufu na hali
tete katika jamii na uchumi duniani kote na ulimwengu wa Kiarabu haukusalimika.
Amesema ingawa
ukanda huo umebarikiwa na mchanganyiko wa mambo na uwezo mkubwa lakini bado
nchi zote ziwe tajiri wa mafuta, za kipato cha wastani au zenye maendeleo duni
zote zinakabiliwa na changamoto ya kukabiliana na janga hili lililoibua athari
zingine “Uchumi wa kanda hiyo umepata mapigo mengi, kuanzia virusi
lakini pia kushuka kwa kasi kwa bei ya mafuta, mapato kutoka nje na utalii.
Matarajio ya kiuchumi ni ya chini kushuhudiwa kwa miaka 50. Na uchumi wa
kikanda utarajiwa kusinyaa kwa zaidi ya asilimia 5 huku katika baadhi ya nchi
ukishuka kwa tarakimu mbili.”
© UNICEF/Delil
Souleiman | Waajiriwa na Wafanyakazi
wakujitolea huko Jirjus wafanya kazi ya kubandika mabango yanayo toa mafunzo
dhidi ya kujikinga na COVID-19.Hii ni kampeni inayofanyika mji wa Qumishly
ilioko kaskazini mashariki kwa Syria.
Ameongeza kuwa
na wakati mamilioni ya watu wakisukumwa chini kiuchumi, robo ya watu wote
katika ulimwengu wa Kiarabu huenda wakaishi katika umasikini.
Katibu Mkuu
amekumbusha kwamba ukanda ambao tayari umeghubikwa na mizozo na pengo la usawa
hali hii itaongeza athari kubwa zaidi za kisiasa na utulivu wa kijamii.
Ametaja
waathirika wakubwa kuwa ni wanawake na wahamiaji ambao wanawasilisha asilimia
40 ya nguvu kazi ya ukanda huo, ambao pia tayari una watu milioni 55
wanaotegemea msaada wa kibinadamu ili kuishi.
Pamoja na
changamoto hizo Guterres amesema COVID-19 inaweza kuwa fursa kubwa kwa
ulimwengu huo kutatua migogoro ya muda mrefu na kushughulikia changmoto za
kimfumo na amependekeza vipaumbele vinne vitakavyowaongoza kujikwamua vyema na
kufikia malengo ya maendeleo endelevu ambavyo ni:-
“Mosi hatua za
haraka za kupunguza kusambaa kwa maambukizi, kukomesha migogoro na kukidhi
mahitaji ya harama ya walio hatarini, Pili kuongeza juhudi za kuzipa pengo la
usawa, tatu kupiga jeki ukwamuaji wa kiuchumi na nne sasa ni wakati wa kutoa
kipaumbele kwa haki za binadamu.”
Amesisitiza
kwamba kwa pamoja ukanda huo unaweza kubadili mgogoro huu kuwa fursa na kuleta
faida kubwa sio tu kwa ukanda huo bali kwa dunia nzima.
No comments:
Post a Comment