World
Bank/Sambrian Mbaabu | Inatarajiwa kwamba miji kama Nairobi Kenya itajikwamua vyema kutokwa kwa
janga la COVID-19.
Wataalam ambao ni wajumbe wa Baraza la ushauri kwa ajili ya masuala
ya kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa (DESA) leo wamechapisha ripoti
inayopendekeza mambo ya kuzingatia kwa ajili ya kujikwamua vyema baada ya janga
la corona au COVID-19 duniani.
Mapendekezo ya
wataaalam hao yanalenga kushauri kuhusu ufikiaji wa malengo yote 17 ya
maendeleo endelevu (SDGs) ifikapo mwaka 2030 huku wakitilia maanani tishio la
milipuko ya majanga na athari zake katika ngazi ya kiuchumi na kijamii.
Miongoni mwa
mapendekezo yaliyowekwa kwenye ripoti na wataalam hao ni pamoja na kuimarisha
ushirikiano wa kimataifa katika masuala ya kodi, kuhakikisha fursa sawa zaidi
katika maendeleo ya teknolojia ya kidijitali, udhibiti endelevu wa maliasili
lakini pia mitazamo yenye thamani katika biashara ya bidhaa.
Pia ripoti yao
pia imeangazia hali ya sintofahamu inayoukabili uchumi wa dunia, kuweka
mwenendo wa uchumi katika historia na kuelezea kwa nini mtazamo maalum wa
maendeleo ya kiuchumi unahitajika.
Mapendekezo
yao pia yametoa wito wa kuongeza msukomo katika masuala ya mazingira katika
kusaka maendeleo ya kiuchumi na kijamii na msukomo zaidi uwekwe katika haja ya
kuwa na ufadhili endelevu na usawa.
Akisisitiza
hilo msaidizi wa Katibu Mkuu katika masuala ya kiuchumi na kijamii Liu Zhenmin
amesema “Katikati ya janga la COVID-19 jumuiya ya
kimataifa imejikuta katika hali isiyotarajiwa na isi yo ya kawaida. Vitisho
vingine vinavyohusiana na afya, uchumi na migogoro ya kijamii vimedhoofisha
nchi na kutuacha njiapanda. Watu masikini wa kutupa na wasiojiweza ndio
walioathirika zaidi wakiwepo ia wanawake na watoto.”
Watu milioni 71
kutumbukia katika ufukara
Mapema mwezi
huu ripoti ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa ya ufuatiliaji wa maendeleo ya
ufikiani wa malengo 17 ya SDGs imeonyesha kwamba ni watu masikini zaidi na
walio hatarini ndio walioathirika vibaya na athari za COVID-19.
Na kukadiria
kwamba takriban watu milioni 71 wanatarajiwa kutumbukia tena katika umasikini
uliokithiri mwaka huu wa 2020 ikiwa ni ongezeko la kwanza la umasikini
kimataifa tangu mwaka 1998.
Kwa upande wa
maendeleo ya teknolojia ya kidijitali watalaam hao wametoa wito wa kuchagiza
utafiti na maendeleo, kuwekeza katika miundombinu na elimu, kuanzisha kanuni za
ufuatiliaji ili kuhakikisha mpangilio wa mikakati inayowekwenda sanjari na
teknolojia inaongeza mishahara hususan kwa wafanyakazi wenye vipato vya chini
na kuboresha usawa wa kiuchumi.
Changamoto za
kidijitali zinaonyesha kiwango cha maamuzi magumu yanayowakabili wafanya
maamuzi katika nia yao ya ukuaji endelevu na ajira zenye hadhi kupitia
mabadiliko ya kimfumo. “Mada hii imekuja wakati muafaka na ni muhimu sana
katika dunia baada ya COVID-19 ambayo itakuwa ni ya kidijitali zaidi yaha po
kabla.” Ameongeza bwana Liu.
Lazima wote
kuongeza juhudi
Mapendekezo
yaliyotolewa na kamati hiyo ya ushauri ya Umoja wa Msataifa ni matokeo ya miaka
miwili ya majadiliano na kazi kubwa iliyofanywa na wajumbe 17ambao wengi wao ni
wanazuoni na watafiti wa masuala ya kiuchumi na pia wanasiasa wafanya maamuzi.
Miongoni mwa
wajumbe hao ni mchumi wa Marekani kutoka chou kikuu cha Columbia Jeffrey Sachs
ambaye amefanyaka kazi kwa miaka mingi kuhusu masuala ya maendeleo endelevu
kwenye Umoja wa Mataifa na Joseph E. Stinglitz mshindi wa tuzo ya amani ya
Nobel katika masuala ya uchumi.
Wakati wa
uwasilishaji wa ripoti ya wajumbe hao Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Amina J. Mohammed amekumbusha kwamba malengo ya SDGs yanasalia kuwa ni mkakati
wa makubaliano kwa ajili ya kujikwamua vyema baada ya COVID-19 ambao unachapuza
mchakato wa vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, umasikini na pengo la usawa
huku ukishughulikia hali ya kutokuwepo na usawa na hatari ambazo zimejitokeza
au kuchangiwa na janga la corona.
Ameongeza
kuwa “hakuna nchi ambayo itaendelea kama tutawaacha watu wengine
nyuma. Ili kujikwamua vyema wote tunahitaji kuongeza juhudi zaidi.” amesisitiza
Bi. Amina Mohammed.
No comments:
Post a Comment