Na: Heri Shaban, Dar es Salaam
JUMLA ya wanachama 274 wamechukua fomu za kinyanyanyiro cha Ubunge Wilaya ya Ilala yenye majimbo matatu ya uchaguzi Ukonga, Segerea na Jimbo la Ilala kushiriki kura za maoni leo Jumatatu.
Akizungumza na waandishi wa habari Wilayani Ilala Leo kwaniaba ya Katibu wa CCM Wilaya hiyo, Mwenezi wa CCM wilaya Alhaj Said Sidde alisema Jimbo la Segerea wamechukua fomu wagombea 95 wanawake 10 na wanaume 85.
Sidde alisema katika Jimbo la Ukonga jumla ya wagombea 146 wote wamechukua fomu kati yao wanaume 123 wanawake 23 na Jimbo la Ilala waliochukua fomu 35 wanaume 28 wanawake 7 na wasiorudisha fomu watatu.
"Katika uchaguzi mkuu wa Wabunge na madiwani mwaka huu mwamko umekuwa mkubwa kwa makada wa chama cha Mapinduzi CCM kuchukua fomu kwasababu ya utendaji kazi mzuri wa Rais John Magufuli katika kujenga Tanzania ya uchumi wa viwanda Watanzania wengi sasa hivi wote wanaunga mkono juhudi za Rais ambapo katika majimbo hayo matatu jimbo la Ukonga limetia fora jumla ya wagombea waliojitokeza ni 146” alisema Sidde.
Sidde alisema katika chaguzi zote ambazo zimefanyika hapa nchini uchaguzi wa mwaka huu umetia fora kwa nafasi za ubunge katika kura za maoni za chama cha Mapinduzi CCM.
Alisema uchaguzi wa kura za maoni CCM kwa Wilaya ya Ilala unatarajia kufanyika Jumatatu Julai 20/2020 na Julai 21/2020 kwa majimbo yote matatu.
Aidha Sidde alisema kwa Jimbo la Segerea uchaguzi utafanyika TABATA katika ukumbi wa Blue Sky eneo la Chuo cha Uhalimu St' Mary's na Jimbo la Ilala utafanyika Ilala LAMADA na Jumanne Jimbo la Ukonga ukumbi wa Lukolo Kitunda Relini.
Aliwataka wapiga kura wote wajumbe wa Mkutano mkuu kufika kwa wakati ili kwenda na ratiba hiyo ya uchaguzi.
No comments:
Post a Comment