Mfanyakazi Bora Robo Ya Nne Ya Mwaka Wa Fedha 2019/2020 Apongezwa - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, July 18, 2020

Mfanyakazi Bora Robo Ya Nne Ya Mwaka Wa Fedha 2019/2020 Apongezwa

Mfanyakazi bora robo ya nne ya mwaka wa fedha 2019/2020 Dkt. Smita Bhalia akipokea Tuzo ya mfanyakazi bora kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati wa hafla fupi ya kumpongeza leo Jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi bora robo ya nne ya mwaka wa fedha 2019/2020 Dkt. Smita Bhalia akipokea mfano wa hundi ya Tshs. Milioni moja kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati wa hafla fupi ya kumpongeza leo Jijini Dar es Salaam.Picha na: JKCI.

Mfanyakazi bora wa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2019/2020 wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Smita Bhalia apongezwa kwa jitihada anazozifanya katika utendaji kazi kwa kufuata sheria na kanuni za utumishi wa umma.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi zawadi mfanyakazi huyo Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi alisema kuwa wafanyakazi wa JKCI wamekua chachu katika kuleta mafanikio ya taasisi hivyo kuifanya taasisi hiyo kukua kwa kasi na kutambulika ndani na nje ya nchi.

“Mfanyakazi huyu bora wa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2019/2020 ni miongoni mwa wafanyakazi mahiri wa JKCI, kutoa zawadi kwake kama mfanyakazi bora ni kuendelea kutoa motisha kwa wafanyakazi wengine wazidi kuchapa kazi” alisema Prof. Janabi

Aidha Prof. Mohamed Janabi amewataka wafanyakazi wa JKCI kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi, kuwahudumia wagonjwa kwa upendo na kujenga mahusiano mazuri baina yao na wagonjwa wanaotibiwa JKCI.

Kwa upande wake Mfanyakazi bora wa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2019/2020 Dkt. Smita Bhalia ameushukuru uongozi wa JKCI pamoja na wafanyakazo wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio yake awapo kazini.

“Ni dhahiri kuwa mimi peke yangu nisingeweza kuwa hapa nilipo, lakini kutokana na ushirikiano uliopo baina yetu wanafamilia ya JKCI ndio ulioniwezesha hata leo kusimama hapa kupongezwa kwa kuwa mfanyakazi bora”,

“Nitaendelea kushirikiana na wafanyakazi wenzangu kutoa huduma iliyo bora kwa wagonjwa wetu kwa kuwa wagonjwa wanatuhitaji sana sisi kama wataalamu wa afya hasa afya ya moyo kuokoa maisha yao”, alisema Dkt. Smita.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages