Wakulima Wa Parachichi Njombe Kuunganishwa na Indonesia - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, July 18, 2020

Wakulima Wa Parachichi Njombe Kuunganishwa na Indonesia



Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Ratlan Pardede alipotembelea bustani ya parachichi ya bwana Nemes iliyopo kata ya Ramadhani mkoani Njombe.


Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Ratlan Pardede alipotembelea moja ya shamba la ufugaji wa samaki na nyuki.


Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Ratlan Pardede alipotembelea kiwanda cha TANWAT kinachozalisha bidhaa mbali mbali zinazotokana na na misitu ikiwemo Mbao na nguzo za umeme.


Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Ratlan Pardede katika ziara yake ya siku mbili mkoani Njombe akihitimisha kwa kukutana na wadau mbali mbali wa maendeleo katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe mkoni Njombe.

Na Amiri Kilagalila, Njombe

Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Profesa Ratlan Pardede amewatembelea wakulima wa parachichi na kiwanda cha kuzalisha nguzo na mbao kupitia kampuni ya Tanwat ambapo ameahidi kuimarisha mifumo ya biashara ya mazao hayo kwa kuanzisha mikakati ya kuwa na biashara za moja kwa moja baina ya Tanzania na Indonesia.

Amesema bei wanayouza parachichi wakulima mkoani Njombe ni mara 6 huko nchini Indonesia hivyo wakulima wamekuwa wakipoteza fedha nyingi kwa kupitisha mazao kwa madalali ambapo ameahidi kuunganisha wafanyabiashara wa nchi zote mbili ili zao hilo liwe na tija.

“Tutaweka karibu zaidi wakulima wa parachichi Njombe na ushirikiano wa watu wa Indonesia”alisema Pardede

Antery Kiwale ni meneja mkuu wa misitu katika kampuni ya Tanwat amesema ujio wa balozi wa Indonesia utasidia kuimarisha masoko ya bidhaa zinazozalishwa huku steven mlimbilila mkulima wa parachichi akisema zao hilo linahitaji usimamizi wa serikali katika kutafta masoko.

“Ujio wa balozi hususani hapa TANWAT na Njombe ni fursa kubwa kujitanua zaidi hasa katika upatikanaji wa masoko ya bidhaa za misitu na kwasasa tunayochangamoto kubwa ya bidhaa zetu kwa mfano mbao”alisema Kiwale Balozi Pardede pia amefanya mazungumzo na wafanyabiashara wa aina mbalimbali mjini Njombe wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini na kuahidi kuyaalika makampuni ya nchini kwake kufanya biashara kwa ukaribu na wafanyabiashara wa mkoani hapa.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages