REA YAWASHA UMEME KWENYE VIJIJI ZAIDI YA 9000 NCHINI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, July 9, 2020

REA YAWASHA UMEME KWENYE VIJIJI ZAIDI YA 9000 NCHINI

Ofisa Uhusiano  wa Wakala wa Nishati Vijijini REA Jaina Msuya (wa katikati) akitoa Elimu kwa mgeni aliyefika kwenye banda lao kwaajili ya kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na REA, kushoto kwake ni Mtaalam wa upimaji wa nguzo Saum Mohamed kutoka katika Kiwanda cha kutengeneza nguzo cha Qwihaya general enterprises company ltd kilichopo Mafinga Iringa, na kulia kwake ni Benedict Marealle kutoka ktoka kwenye kapuni ya Baobab Energy System.
Ofisa Uhusiano  wa Wakala wa Nishati Vijijini REA Jaina Msuya (wa katikati) akitoa Elimu kwa mgeni aliyefika kwenye banda lao kwaajili ya kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na REA, kushoto kwake ni Mtaalam wa upimaji wa nguzo Saum Mohamed kutoka katika Kiwanda cha kutengeneza nguzo cha Qwihaya general enterprises company ltd kilichopo Mafinga Iringa.
Mtaalam wa Upimaji wa nguzo kutoka katika kiwanda cha kutengeneza nguzo cha Qwihaya general enterprises company ltd kilichopo Mafinga Saum Mohamed akitoa ufafanuzi kuhusu ubora wa nguzo zinazozalishwa kwenye kiwanda chao katikati ni Ofisa Uhusiano wa REA Jaina Msuya na wa kwanza kulia ni Ofisa uzalishaji kutoka Benedict Marealle kutoka ktoka kwenye kapuni ya Baobab Energy System.
Mwelimishaji wa Teknolojia ya Sumaku akitoa maelezo kwa watu waliofika kwenye banda la REA katika Maonyesho ya 44 ya Biashara Maarufu kama Sabasaba kujionea Teknolojia hiyo inavyoweza kuwasha jiko la kupikia.
Ofisa kutoka kampuni ya ENVOTEC inayojishughulisha na utengenezaji na usambazaji wa Majiko ya Gesi Salama Sudi akitoa elimu kuhusu ufanisi wa bidhaa ya kwa mwananchi aliefika kwenye banda la REA kujionea shughuli mbalimbali zilizopo kwenye banda hilo katika Maonyesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba.
Bi Regina David Ofisa kutoka kwenye Kampuni inayojihusisha na usambazaji wa Mita maalum zenye uwezo wa kupima ujazo wa Gesi ya KOPA GAS (kushoto), akitoa maelezo kuhusu Mita hizo namna zinavyofanya kazi kwa watu aliefika kwenye banda la REA kujionea shughuli mbalimbali zilizopo kwenye banda hilo katika Maonyesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasab.

Dar es Salaam: Wakala wa Nishati Vijijini REA imesema kuwa hadi kufikia mwezi Juni mwaka 2021 Vijiji vyote vilivyosalia kufikishiwa Umeme vinatakiwa kukamilika kwa kufikiwa na Nishati hiyo.

Ofisa habari wa REA Jaina Msuya amebainishaa hilo kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye Maonyesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba ambapo amesema kuwa mpaka sasa Zaidi ya vijiji 9000 nchi nzima tayari vimefikiwa na Umeme.

Aidha ameongeza kuwa wakati REA inaanzishwa Mwaka 2007 kulikua na Vijiji 502 tu vilivyokuwa na umeme  kati ya vijiji 12,268 nchi nzima, ambapo mpaka sasa zaidi ya Vijiji 300 ndivyo vilivyosalia kupatiwa nishati hiyo na kwamba wanakaribia kutangaza Zabuni kwa wakandarasi ili kuweza kukamilisha kazi hiyo.

“Kuna jumla ya Vijiji 12,268 nchini na tayari zaidi ya Vijiji 9000 vimefikiwa na Umeme sasa imebaki kazi ya kutangaza zabuni kwa wakandarasi ili kuweza kukamilisha kazi hiyo ifikapo mwezi Juni 2021” alisema Ofisa habari huyo Jaina.

Aidha ametoa mwito kwa watu mbalimbali wanaoishi kwenye Vijiji vilivyopatiwa Umeme kuchangamkia fursa hiyo kwa kuanzisha shughuli za uzalishaji mali kwa kuanzisha Viwanda vidogovidogo ili kujiongezea kipato.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages