CRDB WAZINDUA RASMI AKAUNTI YA JUNIOR JUMBO AKAUNTI MKOANI ARUSHA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, April 12, 2021

CRDB WAZINDUA RASMI AKAUNTI YA JUNIOR JUMBO AKAUNTI MKOANI ARUSHA

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro katikati akiwa pamoja na wafanyakazi wa benki ya CRDB mara baada ya kuzindua rasmi akaunti ya mtoto ijulikanayo kama Junior Jumbo Account.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jelly Murro akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki ya CRDB ,wazazi na watoto juzi mara baada ya kuzindua rasmi account ya mtoto ijulikanayo kama [Junior Jumbo account] kutoka CRDB.

Na Woinde Shizza, ARUSHA | Malezi bora katika familia ndiyo msingi wa malezi kwa watoto katika jamii yetu hivyo wazazi wametakiwa kuzingatia kutoa malezi bora kwa watoto wao ndani ya familia na jamii kwa jumla ili kuwa na taifa lenye uchu wa kujiletea maendeleo.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Jelly Murro wakati akizindua account ya mtoto ijulikanayo kama [Junior Jumbo account] kutoka CRDB ambapo alisema wazazi wanawajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora na wawe na utaratibu wa kuwawekea akiba ya pesa kwa ajili ya maisha yao ya badae ili iweze kuwasaidia katika masomo yao na itawajengea maadili mazuri ili kujenga taifa bora lenye watoto wanaojitambua, kujithamini.

Muro alisema wazazi wana wajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora ili kujenga utu, uzalendo na upendo kwa watoto na jamii kwani malezi katika familia ni msingi katika ujenzi wa taifa linalozingatia uzalendo, maadili mema, utu na uwajibikaji katika maendeleo yao na taifa.

unapo muwekea mtoto akiba yake katika benki kwanza inakusaidia wewe mzazi kuwa na uhakikia wa kulipa ada kwa muda wowote pia, mnajua kabisa wazazi mtoto unaporudishwa rudishwa ada unamuathiri kisaikolojia kwani atapata mawazo mengi ambayo yatampelekea hata kushidwa kufanya vizuri darasani” alisema Muro.

Kwa upande wake Neema Njau ambae ni mzazi alisema kuwawekea watoto na vijana akiba ni utaratibu mzuri wa kuweza kuwasadia katika kujiendeleza kielimu na kujenga taifa lenye maadili na upendo.

Kwa upande wake meneja biashara wa kanda David Peter alisema kuwa wanatambua wateja wao wana malengo ambayo wamejiwekea katika maisha yao, na wao kama Benki ya kizalendo wana jukumu la kuhakikisha wateja wanafikia malengo yao kupitia huduma na bidhaa bunifu zinazotolewa na benki ikiwemo huduma ya kuweka akiba kupitia akaunti mbalimbali kama vile akaunti hii ya Junior Jumbo account.

Alisema wanaendelea kuboresha huduma na miundombinu yake ya kutoa huduma hususani ile ya kidijitali, ambapo aliwataka wateja kuwafungulia watoto wao akaunti hii kwani ni mkombozi mkubwa sana kwa mtoto na nimsaada mkubwa pia kwa mzazi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages