MLIPUKO WA VOLCANO MLIMA NYIRAGONGO NCHINI CONGO WALETA MAAFA, NYUMBA 600 ZATEKETEZWA NA MAMIA YA WATOTO HAWAJULIKANI WALIPO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, May 24, 2021

MLIPUKO WA VOLCANO MLIMA NYIRAGONGO NCHINI CONGO WALETA MAAFA, NYUMBA 600 ZATEKETEZWA NA MAMIA YA WATOTO HAWAJULIKANI WALIPO




Na Mwandishi Wetu, Congo DRC | Watu wapatao 11 wanaripotiwa kufa baada ya mlipuko wa volcano katika Mlima Nyiragongo, Mashariki mwa Congo DRC na kiasi cha Kilomita 10 kutoka mji wa Goma ulio na wakazi takriban milioni mbili.

Msemaji wa serikali Patrick Muyaya ameviambia vyombo vya Habari kwamba mamia ya Watoto hawajulikani walipo hadi hivi sasa kwa kupotea ama kupotezana na familia zao baada ya mlipuko huo kutokea Jumamosi jioni.

Muyaya kasema watu watano walipoteza Maisha wakati wakijaribu kuondoka eneo la mlipuko, wakati wafungwa wanne walikufa wakati wakijaribu kutoroka kutoka katika gereza la Munzenze.

Watu wengine wawili wameripotiwa kupoteza maisha siku ya Jumapili.

Mlipuko huo, uliosababisha zaidi ya raia wa DRC 8,000 kukimbilia nchini Rwanda, hivi sasa unaripotiwa kutuama baada ya kuangamiza makazi 600 ya mji wa Goma Pamoja na shule tano.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages