Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Visiwani Zanzibar, SIMAI MOHAMMED SAID, Amesema "Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali, imekiri Kuridhishwa na Fursa za Kimkakati zinazotolewa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na ZSSF kwa ajili ya kuwasaidia Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Kuchangia kwa Hiyari kwa Malengo ya Baadae".
Ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania, Baada ya Kupokea Ripoti Kutoka Kwa Taasisi hizo za Umma. Ni Wakati Sahihi na Muafaka kwa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Kuchangamkia Fursa hizo, zinazolenga kuwakwamua, Amesema.
Mbunge Singida Magharibi, ELIBARIKI KINGU Miongoni mwa Baadhi ya Wabunge Waliohudhuria Mkutano mkuu wa TAHLISO, na Kupata nafasi ya Kutoa Wito kwa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu, Kuhusu Kujiunga na Mifuko ya Hifadhi za Jamii.
Mwenyekiti Mstaafu TAHLISO, PETER NIBOYE akitoa shukrani kwa Taasisi za Umma ikiwemo NSSF kwa kuonesha Dhamira ya Dhati kuwasaidia Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Kufikia Malengo ya Baadae Kupitia Mfumo wa Kujiwekea akiba kwa ajili ya Baadae.
Meneja Uhusiano Elimu kwa Umma Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF LULU MENGELE, akizungumza Wakati wa Mkutano huo amesema, Taasisi hiyo imeandaa mfumo Mzuri Utakaosaidia Wanafunzi Kuchangia kwa Hiyari Bila ya Changamoto Zozote.
Mtangazaji, MASOUD KIPANYA akitoa Wito kwa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu, Kuhusu Kujiunga na Mifuko ya Hifadhi za Jamii na umuhimu wake katika maisha.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Visiwani Zanzibar, SIMAI MOHAMMED SAID (Kulia) akimkabidhi cheti Meneja Uhusiano Elimu kwa Umma Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF LULU MENGELE.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Visiwani Zanzibar, SIMAI MOHAMMED SAID (Kulia) akimkabidhi cheti Mwenyekiti Mstaafu TAHLISO, PETER NIBOYE.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Visiwani Zanzibar, SIMAI MOHAMMED SAID katika picha ya pamoja na Baadhi ya Wabunge walioudhulia Mkutano huo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Visiwani Zanzibar, SIMAI MOHAMMED SAID katika picha ya pamoja na Baadhi ya Viongozi Kutoka Taasisi za Umma walioudhulia Mkutano huo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Visiwani Zanzibar, SIMAI MOHAMMED SAID katika picha ya pamoja na Maraisi kutoka vyuo mbali mbali za Umma walioudhulia Mkutano huo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Visiwani Zanzibar, SIMAI MOHAMMED SAID katika picha ya pamoja na Maraisi kutoka vyuo mbali mbali za Umma walioudhulia Mkutano huo.
No comments:
Post a Comment