UWT YAIPONGEZA STAMICO, YASHAURI WANAWAKE WASHIRIKISHWE SEKTA YA MADINI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, July 9, 2021

UWT YAIPONGEZA STAMICO, YASHAURI WANAWAKE WASHIRIKISHWE SEKTA YA MADINI

Florence Masuka (wa kwanza kulia) Mwenyekiti Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Dar es Salaam akipata maelezo katika Banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

VIONGOZI wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT) kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam wametembelea mabanda mbalimbali yaliyoko katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalim Nyerere.

Miongoni mwa mabanda yaliyotembelewa na viongozi hao wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Tifa ya CCM(NEC) Angel Akilimali ni banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Wakiwa hapo maofisa na watalaam wa STAMICO wa kada mbalimbali walitumia nafasi hiyo kuwaeleza viongozi hao wa UWT shughuli wanazozifanya huku wakionesha wakiwaonesha sampuli za makaa ya mawe ambayo yanatumika kutengeneza mkaa mbadala ambayo yalionekana kuwavutia viongozi hao na kutaka kujua faida zake na jinsi yanavyotumika.

Akifafanua zaidi, sababu za kuamua kutembelea banda hilo la STAMICO, Akilimali amesema pamoja na mambo mengine shirika hilo limekuwa likiendeleza wachimbaji wadogo wa madini na kuwajengea uwezo wa kuchimba madini katika mazingira yasiyo hatarishi kiafya.

"Tunawashuku STAMICO kwa kupata fursa ya kutembelea hapa pamoja na mabanda mengine yaliyomo humu, tumekutana na wajasiriamali wanawake, tumejifunza na kupata uzoefu wao katika shughuli wanazofanya zikiwemo katika sekta ya madini."

"Lakini kwenye sekta ya madini akina mama wengi walikuwa bado waoga wanaogopa, walikuwa hawana muamko, hivyo kwa kutembelea kwetu tukitoka hapa tunakwenda kuhamasisha wanawake wa UWT ili waweze kukimbilia fursa hiyo."

"Wanawake wasiogope kwani wanaweza, na kama katika mabanda hayo ya madini kuna wanawake ambao wameweza basi na wanawake wengine wanaweza, hivyo ni kuchangamkia fursa kwa kujitokeza kufanya shughuli za uchimbaji madini," amesema.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages