RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATOA ZAIDI YA SH. 2 BILIONI KUWATUA NDOO WANAWAKE TARAFA YA KISIRIRI IRAMBA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Saturday, April 2, 2022

demo-image

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATOA ZAIDI YA SH. 2 BILIONI KUWATUA NDOO WANAWAKE TARAFA YA KISIRIRI IRAMBA

IMG_3132
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda (wa pili) akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Wagonjwa Mahututi (ICU) linalojengwa Hospitali ya Wilaya Kiomboi mkoani Singiga juzi. Kulia ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Kiomboi Abel Mafuru.
IMG_3138
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kiomboi Abel Mafuru akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo.
IMG_3143
Wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya huo wakiwa kwenye ukaguzi wa jengo hilo.
IMG_3152
Mhandisi wa Wilaya hiyo, Profiri Modaha akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo.
IMG_3155
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungumzia ujenzi huo wakati wa ukaguzi.
IMG_3165
Wajumbe wa kamati hizo wakikagua matengenezo ya barabara ya Old Kiomboi-Kisinda na Doromoni.
IMG_3166
Meneja wa TARURA Wilaya ya Iramba Mhandisi Evance Kibona akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo.
IMG_3181
Mjumbe wa kamati hiyo, Edward Makala akichangia jambo wakati wa ukaguzi wa barabara ya Kiomboi-Ruruma-Uwanza.
IMG_3190
DC wa Iramba Suleiman Mwenda akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo. Kulia ni Meneja wa TARURA Wilaya ya Iramba, Mhandisi Venance Kibona.
IMG_3199
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, David Madelu akichangia jambo wakati wa ukaguzi wa mradi wa upelekaji umeme Kijiji cha Tutu.
IMG_3207
Muonekano ya vyumba vya maabara katika Shule ya Sekondari ya New Kiomboi.
IMG_3212
Ukaguzi wa ujenzi wa Maabara Shule ya Sekondari ya New Kiomboi ukifanyika.
IMG_3214
Mkuu wa Sekondari ya New Kiomboi Amadeus Kiduu akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba viwili vya maabara.
IMG_3225
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda (kulia) akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya New Kiomboi wakati wa ukaguzi wa vyumba vya maabara.
IMG_3229
Ukaguzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kisiriri ukifanyika.
IMG_3234
Kamati hiyo ikipokea maelezo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kisiriri kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya Iramba Hussein Sepoko (kulia).
IMG_3239
Muonekano wa kituo cha Afya cha Kisiriri.
IMG_3250
Ukaguzi wa Mradi wa Maji Kijiji cha Kisiriri ukifanyika.
IMG_3252

Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Iramba Mhandisi Ezra Mwacha akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo.
IMG_3256
Ukaguzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Tyegelo ukifanyika.
IMG_3264
DC Mwenda akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa kituo hicho cha Afya.
IMG_3268
Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Beatrice Mashausi akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho.
IMG_3279
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kidaru Kyegelo.
IMG_3283
Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba, Pius Sangoma akizungumza wakati akiwatambulisha viongozi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa hadhara katika kijiji hicho.
IMG_3289
Mkutano ukiendelea.
IMG_3291
Kaimu Katibu wa CCM wa wilaya hiyo katika ziara hiyo ya ukaguzi ambaye pia ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi, Johari Selemani akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara ambapo aliwasihi wanachama wa chama hicho kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa ndani utakaofanyika hivi karibuni.
IMG_3302
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akihutubia kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale, Singida

ZAIDI ya Sh.Bilioni 2 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan katika mwaka mmoja wa uongozi wake zimewawezesha Wanawake wa Tarafa ya Kisisiri iliyopo Wilaya ya Iramba mkoani hapa kuwatua ndoo za maji baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji uliotekelezwa kutokana na fedha hizo.

Kabla ya kutekelezwa kwa mdari huo wanawake hao walikuwa na adha kubwa na kutumia muda mwingi kutembea umbali mrefu kutafuta maji ya visima vya kuchimba kienyeji huku wakiwa hawana uhakika wa kuyapata maji hayo ambayo hayakuwa salama kwa matumizi ya kunywa.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda wakati akiwahutubia wananchi wa Tarafa ya Kisiriri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Didaru baada ya kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo kumaliza ziara ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo katika Tarafa hiyo juzi.

Mwenda alisema kamati hizo zilifanya ukaguzi wa miradi hiyo ili kuona nini kimefanyika katika mwaka mmoja wa uongozi wake Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.

Mwenda aliitaja miradi walioitembelea na kuikagua kwa sekta ya elimu kwa Shule za Msingi kuwa ni ukamilishaji wa darasa moja katika Shule ya Msingi Kiomboi Hospitali ambapo walipokea Sh.11,363,636.40, ukamilishaji wa darasa moja Shule ya Msingi Kisimba ambao pia walipokea Sh.11,353,636.36 ambao ujenzi wake umefikia hatua ya lenta ambao unatekelezwa kwa nguvu ya Wananchi.

Halikadharika Mwenda alitaja miradi mingine kuwa ukamilishaji wa darasa moja katikaShule ya Msingi Tulya kwa gharama ya 11,363,636.36, ukamilishaji wa ujenzi wadarasa moja Shule ya Msingi Doromoni kwa kiasi hicho hicho cha fedha kilichotolewa Shule ya Tulya ambapo jumla ndogo ya miradi hiyo ikiwa ni Sh.45,454.,545.48.

Akiitaja miradi ya Shule za Sekondari iliyotekelezwa kuwa ni ujenzi wa chumba kimoja cha darasa Shule ya Sekondari Kisiriri ambao umetumia Sh.20,000,000, ukamilishaji wa vyumba viwili vya maabara katika Shule ya Sekondari ya Kisana ambapo walipokea Sh.30,000,000 na ukamilishaji wa vyumba vingine viwili vya maabara katika Shule ya Sekodari ya New Kiomboi kwa gharama hiyohiyo na kuifanyajumla ndogo kuwa ni Sh.60 Milioni.

Akielezea Sekta ya Afya alisema wamejenga Kituo cha Afya Kisiriri kwa gharama ya Sh.250,000,000 na kuwa ujenzi wake upo katika hatua ya umaliziaji jengo la OPD likiwa kwenye hatua za upakaji wa rangi, kuwekwa milango na madirisha na halikadharika jengo la maabara.

Alitaja mradi mwingine wa sekta ya Afya kuwa ni ujenzi wa Kituo cha Afya Tyegelo ambao pia walipokea Sh.250,000,000, ujenzi wa choo Zahanati ya Doromoni ambao unatekelezwa kwa gharama ya Sh.40,000,000, ujenzi wa choo Zahanati ya Kisana kwa gharama ya Sh.39,950,000 jumla ndogo yake ya ujenzi wa vyoo hivyo ikiwa ni Sh.79,950,000 huku ujenzi wa Zahanati ya Tutu ukigharimu Sh. 50,000,000.

Mwenda aliongeza kuwa katika Sekta hiyo ya Afya wanakamilisha ujenzi wa wodi ya dharura (EMD) katika Hospitali ya Wilaya ambapo wamepokea Sh.300,000,000, ujenzi wa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) kwa gharama ya Sh.250,000,000 huku jumla yake ndogo ikiwa ni Sh.550,000,000.

Aidha Mwenda akizungumzia Sekta ya barabara alisema wanafanya matengenezo ya barabara ya Kisiriri-Kisimba kilometa 9.42, Old Kiomboi-Meli-Walla-Ntwike kilometa 0.9, matengenezo ya kawaida barabara ya Kitusha-Kisana Kilometa 6.0 na ujenzi wa mifereji mita 100 kwa gharama ya Sh.126,383,800.

Alitaja mradi mwingine kuwa ni matengenezo muda maalum barabara ya Kiomboi-Ruruma-Uwanza kilometa17.4 kwa gharama ya Sh.492,019,500, matengenezo muda maalum barabara ya Old Kiomboi-Kisimba-Doromoni Kilometa 9 na kufungua barabara ya Kibigiri Masagi-Kinkungu na kufungua barabara ya Migilango kilometa 5 na na Barabara ya Mwamapuli- Luono ambazo zote kwa pamoja jumla yake kuu ni Sh. 1,295,947,201.

Alisema mradi mwingine walioukagua ni upelekaji wa umeme kwenye kitongoji cha Tutu ambao unatekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa gharama ya Sh.122,331,420.54 ambao umekamilika kwa asilimia 100.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara hiyo Mwenda alisema miradi hiyo inafanyika ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali inawajibu wa kuikagua ili kuona kama inatekelezwa kwa viwango vinavyo hitajika.

Mwenda alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo na kuwaomba viongozi ilipo miradi hiyo kuwahamasisha wananchi wao kuitunza.

Aidha Mwenda aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa vijana wanaoshiriki katika zoezi la anuani za makazi na postikodi linaloendelea nchi nzima kwa kuwaelekeza majina ya mitaa na mambo mengine yanayohitajika na akawaomba kufanya hivyo pia katika zoezi la Sensa ya watu na makazi.

Ziara hiyo ambayo imeleta ari na mwamko mkubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo kushiriki shughuli za maendeleo baada ya kupokea taarifa ya miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ambapo pia walitumia nafasi hiyo kumpongeza pamoja na mbunge wao Dk.Mwigulu Nchemba kwa kutoa fedha nyingi ilifanyika katika Tarafa za Ndago, Kinampanda, Shelui na Kisiriri zenye jumla ya kata 20 na vijiji 70.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *