UGUMU WA MAISHA UNATOFAUTIANA, TUENDELEE KUSAIDIANA – MHE.OTHMAN - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Thursday, April 21, 2022

demo-image

UGUMU WA MAISHA UNATOFAUTIANA, TUENDELEE KUSAIDIANA – MHE.OTHMAN

WhatsApp%20Image%202022-04-21%20at%205.28.14%20PM
WhatsApp%20Image%202022-04-21%20at%205.25.54%20PM
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa Bi.Khadija Khamis Faki wa Kijiji cha Kiuyu Minungwini Wilaya ya Wete- Pemba wakati Mhe. Othman alipokuwa katika ziara maalum ya kuwafariji na kuwapa pole wafiwa, wajane, wagonjwa na watu mbali mbali wasiojiweza wilayani humo, Mhe. Othman alifika kijiji hapo kumjulia hali Bi Fatma Khatib Juma (ambaye ni Mama mzazi wa Khadija) April 21,2022.
WhatsApp%20Image%202022-04-21%20at%205.24.20%20PM
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, akisalimiana na Mzee Bakari Khalfan Mazimbe wa Kijiji cha Tumbe wilaya ya Micheweni wakati Mhe. Othman alipofika nyumbani kwa Mzee Mazimbe huko Tumbe kumjulia hali akiwa katika ziara maalum ya kuwafariji na kuwapa pole wafiwa, wajane, wagonjwa na watu mbali mbali wasiojiweza wilayani humo, April 21,2022.
WhatsApp%20Image%202022-04-21%20at%205.22.19%20PM
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, akifurahia jambo na Mzee Hamad Faki Othman wa Kijiji cha Mjini Wingwi Wilaya ya Micheweni wakati Mhe. Othman alipofika nyumba kwa Mzee Hamad kumjulia hali akiwa katika ziara ya kuwafariji na kuwapa pole wafiwa, wajane, wagonjwa na watu mbali mbali wasiojiweza wilayani humo, April 21,2022. (Picha na Kitengo cha Habari Ofisi ya makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar)

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema kuwa wananchi hapa visiwani, wameelemewa na viwango tofauti vya ugumu thakili wa maisha, licha ya ulimwengu mzima sasa kukabiliwa na hali hiyo.

Mheshimiwa Othman ameyasema hayo leo, katika Kijiji cha Tumbe-Rahaleo, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, akisalimiana na viongozi na wananchi mbali mbali, waliojitokeza kumpokea, akiwa katika Ziara yake Maalum ya Siku Nne, kisiwani hapa.

Hiyo ni sehemu pia ya salamu za Mheshimiwa Othman, akikamilisha Ziara yake katika Mikoa yote Mitano na takriban Majimbo 50 ya Unguja na Pemba, alipowatembelea na kuwajulia hali, pamoja na kujumuika nao katika Iftari, wananchi mbali mbali wanyonge na wahitaji wakiwemo wajane, yatima na wazee wasiojiweza, tangu mwanzoni kabisa mwa mwezi huu.

Amesema kuwa, kubaini viwango vya hali duni ya maisha magumu yanayowasibu wananchi waliowengi, ni vyema kuwafikia, kuwatembelea ana kwa ana, na hatimaye ikibidi kuwafikiria kwa kuwatafutia namna bora ya kuwasaidia kwa hali na mali, ili kuwawekea mazingira angalau ya kujikimu katika Misimu hii ya Kheri, hasa ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Ndugu zangu uzito wa ugumu wa maisha ni wa viwango tofauti mathalan ujazo wa kilo tano na wengine kilo kumi na zaidi kwa kuendelea”, amesisitiza Mheshimiwa Othman ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo–Zanzibar.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba, Bw. Hamad Omar Bakar ‘Small’, ameeleza hali ya faraja na matumaini mema waliyokuwa nayo wananchi, hasa pale walipomuona Mheshimiwa Othman na Viongozi wengine, wakikata mitaa, ‘jua-mvua’ ili kuwafikia wanyonge, hata iwapo mazingira yalikuwa magumu kupita kiasi.

Katika ziara yake hiyo, Mheshimiwa Othman alijumuika na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Jamii, Masheha wa baadhi ya Shehia, Vyama vya Siasa, na Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakiwemo Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote za Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *