DCI afunga mafunzo ya I-EAC jijini Dodoma - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, May 13, 2022

DCI afunga mafunzo ya I-EAC jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCI Camilius Wambura amesema Jeshi la Polisi nchini limejipanga kuhakikisha kuwa hakuna mhalifu anayetamba hapa nchini na wanaofanya uhalifu wataendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria kwakushirikiana na taasisi nyingine ikiwemo Shirikisho la Polisi wa Kimataifa (INTERPOL).

DCI Wambura ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa ufungaji wa mafunzo ya mradi wa INTERPOL EAST AFRICA COMMUNITY (I-EAC) kwa Watendaji wa Taasisi mbalimbali watakaohusika na mradi huo ambao lengo lake ni kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka.

Kwa upande wake Mshiriki wa Mafunzo hayo kutoka Wakala wa Usajili ufilisi na udhamini (RITA) ROBBY OTAIGO amesema mafunzo hayo yatawajenga kushirikiana na INTERPOL katika kupambana na uhalifu huku Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Kenya Bi. ALLEN BAMBAZI akisema wanatarajia kuongeza muda wa mafunzo hayo ili kuwafikia watu wengi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages