WAZIRI PROF. ADOLF MKENDA ATEMBELEA BANDA LA MAMLAKA YA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, May 27, 2024

WAZIRI PROF. ADOLF MKENDA ATEMBELEA BANDA LA MAMLAKA YA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Tanzania, Mhe. Prof. Adolf Mkenda Jumatatu ya tarehe 27.05.2024, Ametembelea Banda la Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar na kuweza kupata maelezo ya kina kuhusu Bunifu zilizofanywa pamoja na kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Mafunzo ya Amali,, ambapo maelezo hayo yalitolewa na Mkurugenzi Vyuo na Mafunzo wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Mhandisi Abdllah Mohamed Hambaly, Alipofika kutembelea katika Banda la Maonesho la MMA katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu, yanayofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Popatlal Jijini Tanga.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Tanzania Mhe. Prof. Adolf Mkenda pamoja na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi wakipata maelezo kutoka kwa kwa Mkurugenzi Vyuo na Mafunzo wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhandisi Abdalla Mohamed Hambal (wa kwanza kulia) walipotembelea banda la Mamlaka ya Mafunzo ya Amali, kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika jijini Tanga katika viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Tanzania Mhe. Prof. Adolf Mkenda akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Vyuo na Mafunzo wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhandisi Abdalla Mohamed Hambal (wa kwanza kulia) alipotembelea banda la Mamlaka ya Mafunzo ya Amali , kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika jijini Tanga katika viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages