IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR YAWAAGA WASTAAFU - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, June 21, 2024

IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR YAWAAGA WASTAAFU

Mwenyekiti wa Bodi ya Idara Habari Maelezo Yussuf Omar Chunda akimkabidhi Zawadi ya Fedha Taslim aliekua Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Hassan Khatibu Hassan katika hafla ya kuwaaga Wastaafu wa Idara hio hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

Na: Sabiha Khamis, Maelezo-Zanzibar

Mwenyekiti wa Bodi ya Idara Habari Maelezo Zanzibar Yussuf Omar Chunda amewataka wafanyakazi kuwa na nidhamu wanapokuwa kazini ili kuwajengea heshima wanapofikia kustaafu.

Wito huo ameutoa katika hafla fupi ya kuwaaga wafanyakazi wawili wa Idara hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo amesema nidhamu inapodumu kwa mfanyakazi hupelekea mashirikiano mazuri kwa wafanyakazi wengine.

Aidha amewataka wastaafu hao kuendelea kutoa mashirikiano kwa pale ambapo wanahitajika kwa ushauri na mapendekezo iwapo wakiwa nje ya ofisi

Ameeleza kuwa wafanyakazi waliobakia kazini wanapaswa kufuata nyayo za wastaafu hao kwa kufanyakazi kwa weledi ili kupatikana ufanisi.

Nae, Katibu Mkuu wa Vyama vya Wafanyakazi Khamis Mwinyi Mohamed amewaomba wafanyakazi kujiunga na umoja wa vyama vya wafanyakazi jambo ambalo litawasaidia kutatua changamoto zao.

Ameeleza kuwa Umoja ndio daraja la kupatikana kwa fursa ambazo zitawawezesha Wafanyakazi kushiriki katika kutoa changamoto zao kujadili mambo yao mbali mbali wanayokumbana nayo katika sehemu zao za kazi ili kupatiwa msaada.

Wafanyakazi wakipata changamoto kazini Chama cha Wafanyakazi ndio watetezi wao tunahakikisha inapatikana suluhisho la tatizo hilo” amesema Katibu Khamis.

Hata hivyo ameishukuru Idara hiyo kwa kuwaunga mkono vyama vya wafanyakazi katika kutatua changamoto za wafanyakazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mstaafu wa Idara Habari Maelezo Zanzibar Hassan Khatib Hassan amewashukuru Viongozi wa Idara hiyo kuendeleza utamaduni wa kuwaaga wafanyakazi wake wanapostaafu jambo ambalo huwapa moyo na faraja.

Aidha amesisitiza nidhamu, uadilifu na heshima katika kazi na kuwataka wafanyakazi kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi ili wanapostaafu waweze kujiendeleza.

Chama cha Wafanyakazi kimemkabidhi cheti cha heshima cha uchangiaji bora Mfanyakazi Sikudhani Said ambae amechangia kwa miaka 40.
Mwenyekiti wa Bodi ya Idara Habari Maelezo, Yussuf Omar Chunda akimkabidhi Cheti cha Utumishi Bora Skudhani Said Mbwana aliyekua kitengo cha Ufundi na Vipaza sauti (P. A) Idara Habari Maelezo katika hafla ya kuwaaga Wastafu waliotumikia Idara hio hafla iliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Aliyekua Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Hassan Khatibu Hassan ambaye ni Mstaafu akizungumza katika hafla ya kuwaaga wastahafu wa Idara hio katika hafla iliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi ya Idara Habari Maelezo, Yussuf Omar Chunda akizungumza katika hafla ya kuwaaga waliokua Wafanyakazi wa Idara hio, Hassan Khatibu Hassan aliyekua Mkurugenzi na Skudhani Said Mbwana aliyekua kitengo cha Ufundi na Vipaza sauti (P.A) hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Afisa Utumishi Mkuu Wizara ha Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Subira Mtumwa Haji akitoa nasaha zake katika hafla ya kuwaaga wastahafu wa Idara Habari Maelezo Hassan Khatibu Hassan aliekua Mkurugenzi na Skudhani Said Mbwana aliekua kitengo cha Ufundi na Vipaza sauti (P. A) hafla iliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

(Picha na Yussuf Simai - Habari Maelezo Zanzibar)

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages