Siti Amekutana na Masheha Kujadili Ukatili na Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto Wilaya ya Kati Unguja - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, June 14, 2024

Siti Amekutana na Masheha Kujadili Ukatili na Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto Wilaya ya Kati Unguja

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Siti Abasi Ali akizungumza na Masheha wa Wilaya ya Kati kuhusiana na mikakati ya kupambana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na Watoto, huko Dunga Mkoa wa Kusini Unguja.
Katibu wa Masheha Wilaya ya Kati Zidi Suleiman Abjeid akichangia katika kikao cha kujadili mikakati ya kupambana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na Watoto, huko Dunga Mkoa wa Kusini Unguja.
Sheha wa Shehia ya Bambi Amour Pandu Mkombe akichangia katika kikao cha kujadili mikakati ya kupambana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na Watoto, huko Dunga Mkoa wa Kusini Unguja.

Na.Takdir Ali, Maelezo-Zanzibar

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Siti Abasi Ali amewaomba Masheha wa Wilaya ya Kati kuwatafuta wamiliki wa Maboma ya nyumba na nyumba za kukodisha katika Shehia zao ili kuziba myanya ya vitendo viovu katika jamii.

Ameyasema hayo huko Dunga Wilaya ya Kati wakati alipokuwa akizungumza na Masheha hao pamoja na kujadili mbinu mbalimbali, zitakazoweza kuondosha vitendo hivyo na Watoto kubaki salama mitaani.

Amesema baadhi ya majengo hayo katika Shehia hizo yamekuwa yakitumika kufanyia vitendo hivyo vinavyoathiri jamii.

ni vyema kuendelea kushirikiana kuweka mikakati ya kuondosha viashiria vinavyosababisha masuala ya udhalilishaji ili kuwakinga Wanawake na Watoto kutokana na viendo hivyo.” alisisitiza mkurugenzi Siti.

Aidha amewataka masheha hao kushirikiana kikamilifu na Waratibu wa jinsia katika shehia zao ili malengo yaliopangwa na Serikali ya kupiga vita vitendo vya udhalilishaji yaweze kufikiwa.

Nataka niwapongeze kwa dhati Waheshimiwa Masheha, munafanya kazi kubwa na ngumu lakini tunakuombeni muzidishe mashirikano na Waratibu wetu kwani tumewapa mafunzo ya kutosha na wanaleta ripoti kila baada ya miezi mitatu.” Alisema Mkurugenzi Siti.

Mbali na hayo Siti amewaomba Masheha hao kusimamia kuanzishwa Majukwaa ya Wanawake Wajasiriamali katika Shehia zao ili waweze kupata fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo Mikopo.

Kwa uapande wake Katibu wa Masheha wa Wilaya ya Kati Zidi Suleiman Abjeid amesema wataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Waratibu hao licha ya kazi ngumu wanayoifanya usiku na mchana.

Hata hivyo ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo waliopewa na Mkurugenzi huyo ili kuondoa Janga la udhalilishaji kwa faida ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Nao baadhi ya Masheha wa Shehia za Wilaya ya Kati wameomba kutatuliwa changamoto zinazowakabili ikiwemo kupatiwa posho la usafiri.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages