SITI ASHAURI KUANZISHWA DAWATI LA JINSIA BANDARINI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, June 7, 2024

SITI ASHAURI KUANZISHWA DAWATI LA JINSIA BANDARINI

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Siti Abas Ali akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Bw. Akif Ali Khamis kuhusiana na kuanzisha Dawati la Jinsia Bandarini huko katika Ofisi za Shirika hilo Malindi Mjini Zanzibar.

Na Takdir Ali-Maelezo, Zanzibar

Idara ya maendeleo ya ya Jamii, Jinsia na Watoto inatarajia kuanzisha Dawati la Jinsia katika eneo la Bandari ili kuondosha matatizo yanayojitokeza.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Idara hiyo, Siti Abasi Ali wakati alipofanya ziara na mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar huko Ofisi za Shirika hilo Malindi Mjini Zanzibar.

Amesema lengo la kufanya ziara hiyo ni kujadili na kupata njia za kuweza kuanzishwa Dawati hilo ambalo litasaidia kuondosha chanagamoto zinazojitokeza kwa Wanawake.

Aidha Siti ameshauri kuwekwa kwa vifaa maalum vya wanawake katika vyombo vya kusafiria ili wanawake wanapopata masuala yao kwa dharura waweze kujisitiri.

Hata hivyo amesema Dawati hilo pia litasaidia kwa mtu anaefanyiwa udhalilishaji akiwa Bandarini au katika Boti kujuwa sehemu sahihi ya kupeleka taarifa zao.

Mara nyingi tunapoingia katika maboti tunaona wahudumu wanawake wapo zaidi katika vyumba vya watu mashuhuri (VIP) lakini hizo sehemu nyengine wanakaa wahudumu wa kiume hivyo mwanamke akipata dharura yoyote ya kijanajike inakuwa ngumu kuenda kumwambia mwanamme, tunataka wawepo Wanawake wenzetu.” alisema Mkurugenzi huyo.

Mbali na hayo amewapongeza Wamiliki wa vyombo vya Baharini kwa kuweka utarajibu maalum wa kusajili Watoto wanaoingia ndani ya Boti sambamba na kuwahudumia vizuri Watu wenye ulemavu ikiwemo kuwapelekea vigari vya maringi matau jambo ambalo linawapa faraja.

Kwa uapnde wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Bw. Akif Ali Khamis amesema wazo la kuanzishwa Dawati la jinsia Bandarini ni zuri kwani kuna Abiria zaidi ya milioni 3 wanaosafiri na wengi wao ikiwa ni wanawake.

Amesema shirika la Bandari linauwiano nzuri kati ya Wafanyakazi Wanawake na Wanaume hivyo watakaa pamoja na taasisi zinazohusiana na Bandari ili kuweza kulifanyia kazi suala hilo kwa faida ya Wanawake na Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages