TAIFA STARS YAIFUATA ZAMBIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA JUMANNE NDOLA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, June 9, 2024

TAIFA STARS YAIFUATA ZAMBIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA JUMANNE NDOLA

KIKOSI cha timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimeondoka leo asubuhi kwenda Jijini Ndola nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya wenyeji, Chipolopolo Jumanne kuanzia Saa Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola.

Wapinzani wengine wa Taifa Stars Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 ni Morocco, Niger, Kongo na Eritrea ambayo imejitoa katika mbio za kuwania tiketi ya Fainali hizo zinazoandaliwa kwa pamoja na Canada, Mexico na Marekani.

Taifa Stars ilianza vyema kampeni zake za Kombe la Dunia 2026 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Niger Novemba 18 mwaka jana Uwanja wa Marrakech nchini Morocco, bao pekee la mshambuliaji mzaliwa wa DRC, Kokola Charles William M'Mombwa wa Macarthur FC ya Australia.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages