Uchumi Wa Bluu Wahitaji Kuwa Na Ushirikiano Kwa Serikali Mbili - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, June 23, 2024

Uchumi Wa Bluu Wahitaji Kuwa Na Ushirikiano Kwa Serikali Mbili

Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi Dkt.Khalid Salum Mohamed akizungumza na katika Banda la Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA) katika Maonesho na Maadhimisho ya Siku ya Mabaharia yanayoendelea katika viwanja Shule Njema wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

*Kuna maeneo mengine ya uchumi wa Bluu hajaangaziwa

Na Chalila Kibuda, Bagamoyo

Waziri Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Zanzibar, Dk Khalid Salum Mohamed amesema kuwa Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zinatakiwa kuwa na ushirikiano kwenye uchumi wa Bluu.

Dkt.Khalid ameyasema katika kulekea maadhimisho na Maonesho Siku ya Mabaharia Duniani ambayo hufanyika kila mwaka Juni 25 na Tanzania yanafanyika wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Maadhimisho yameandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA).

Amesema kuwa katika uchumi huo wa Mabaharia ni nguzo muhimu katika usafirishaji wa abiria na mizigo.

Amesema kuwa Mabaharia wanapitia changamoto nyingi katika kazi hizo lakinj Serikali zimeweka mazingira mazuri katika kutatua changamoto zao.

Amesema fursa uchumi wa bluu zitizamwe zaidi na wananchi washirikshwe kujua Serikali zao zinafanya nini kwenye uchumi huo.

Dkt.Khalid amesema jitihada za makusudi zinapaswa kufanywa ili kuziendeleza fursa mbalimbali za uchumi wa Bluu ambao haujaangaziwa.

Dk Khalid amesema katika Maonesho hayo waweeleze wananchi juu ya umuhimu Sekta ya Bahari na Mabaharia na kuwaeleza wanafunzi kuhusiana na kazi ya Mabaharia ili kuwaongezea kitu kipya katika kupenda fani hiyo.

Dkt. Khalid amesema agenda ya uchumi wa Bluu duniani unashika kasi lakini hapa nchini bado maeneo mengi kama ya utalii hayajatizamwa vizuri na kuwekezwa ikiwa wataalamu watavibainisha na kuweka kwenye maandiko.

"Fursa zipo nyingi sana lakini kwa bahati mbaya hatujazitumia ipasavyo na kuongeza Serikali zote mbili zinapaswa kuzifanyia kazi na jambo hilo linawezekana," amesema Dk Khalid.

Dkt.Khalid akitoa moja ya mfano wa A Zanzibar akisema watu wanajua visiwa vya Unguja na Pemba lakini kuna visiwa vingine vidogo vidogo 44 ambavyo vimekaa tu lakini sasa tumeanza kuvifanyia kazi na kati ya hivyo 17."

Amesema katika moja ya hivyo 17 inajengwa hoteli ya kisasa na wavuvi hawakuondoshwa bali wameboreshewa mazingira.

Amesema Pemba kuna chumba chini ya bahari, ukiwasha taa samaki wanakuja, usingizi unakuwa burudani kabisa na kutokana na umuhimu wa chumba kile, ukitaka kukipata unaweka oda mwaka mzima. Huu ndio uchumi wa bluu tunaoutaka," amesema

Amesema eneo jingine linaloweza kufanyiwa kazi ni kuangalia maunganisho ya Bagamoyo na Unguja kwa sababu ni dakika 45 tu, watalii wakafanya utalii Bagamoyo kisha wakaenda Zanzibar:"Hili nalo ni moja ya uchumi wa bluu tunaopaswa kufanyia kazi."

Dk Khalid amesema Meli ya MV Mapinduzi ambayo itakuwa inafanya safari zake Unguja- Pemba- Dar es Salaam na Tanga iko mbioni kuanza kazi baada ya matengenezo yake kukamilika.

Amesema hali kama hiyo iko Ziwa Victoria ambapo Serikali ya Jamhuri inaendelea kuboresha usafiri majini.

Dkt. amesema mwaka 1974 Serikali ilijiunga na Shirika la Baharia Duniani (IMO) tulijiunga kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wizara hizi ni muundo tu lakini ni suala la Muungano.

Aidha amesema suala la usafiri majini ndio usafiri mkuu kwa sababu ndio unasafirisha mizigo kwa zaidi ya asilimia 90. Tunapozunguza baharia huku ndio tunazungumzia maisha yetu.

"Tulipopata tatizo la Uviko-19 mwaka 2021, meli zikashindwa kusafirisha mizigo kila mmoja alishuhudia maisha yakipanda katika kipindi kwa hiyo maadhimisho siku muhimu sana katika maisha ya binadamu," amesema.

"Hawa mabaharia wanafanya kazi kubwa sana. Tuna kila sababu kuwashukuru na kuwapongeza. Kazi ni wito na bila ninyi hali ingekuwa ngumu sana," amesema.

Amesema safari za Mabaharia majini zinachukua muda mrefu hivyo kuwafanya kukaa mbali na familia, watoto, ndugu, jamaa na rafiki na huko wanakutana na changamoto nyingi huko baharini.

"Usalama Mabaharia ni kitu muhimu na lazima tuhakikishe tunaweka mazingira sawa kwanza wasafiri salama na wanapata haki zao zinazostahili. Serikali zote mbili zitafanya kila linalowezekana maslahi yenu yaendelea kuboreshwa," amesema.

Amesema hilo litafanyika ili kutekeleza mikataba mbalimbali 25 ambayo nchi imeingia duniani ikiwemo mkataba wa kazi, mkataba wa kimataifa wa usalama wa maisha baharini, mkataba wa viwango vya mabaharia na mkataba wa utafutaji na uokoaji.

"Mikataba yote hii na mingine, Serikali zote mbili inazifanyia kazi kwani uchumi wetu unategemea usafiri huo," amesema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amesema anafahamu umuhimu wa maonyesho haya:"Nitoe rai kwa wananchi kuja kujifunza, shule kuleta wanafunzi ili kuja kujifunza na kujua kazi za ubaharia kwani msingi wake huanzia chini."

Kunenge amesema Pwani ndio mkoa unaoongoza kwa viwanda vingi Tanzania. Mpama sasa kuna viwanda 1553 kati ya hivyo 124 ni vikubwa na 34 ni vipya vimejengwa hivi karibuni na vingine vinaendelea kujengaa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA), Sheikha Ahmed Mohamed amesema kila Juni 25 huwa ni siku ya mabaharia na Tanzania huanza na maadhimisho kuanzia Juni 22 kwa kutoa elimu na maonesho kwa wananchi.

Amesema katibu Mkuu wa IMO amezitaka nchi mbalimbali kutambua umuhimu wa mabaharia kwani asilimia 90 ya mizigo inayosafirishwa inategemea mabaharia.

"Ni wajibu wetu kulinda maslahi ya mabaharia, kuwalinda na usalama kwani bila mabaharia hakuna usafirishaji, hakuna manunuzi," amesema Sheikha

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA), Sheikha Ahmed Mohamed akitoa maelezo ya maadhimisho hayo amesema kila Juni 25 huwa ni siku ya mabaharia na Tanzania huanza na maadhimisho kuanzia Juni 22 kwa kutoa elimu na maonesho kwa wananchi.

Amesema katika maadhimisho hayo hatuna budi kuyatathmini maisha ya mabaharia na kuyahadithia kama kauli mbiu yetu ya mwaka huu inavyotaka tuzingatie usalama wao kwanza ili tuwalinde na kuwajengea mustakabali mzuri wa maisha yao ya baadae.

Amesema tunaelewe kazi ya ubaharia ni kazi nzuri na yenye tija kwa mabaharia wenyewe na jamii kwa jumla, kwani inatoa fursa nyingi ambazo baharia anaweza kuzipata na hivyo kujijenga vizuri kiuchumi na kielimu.

"Hata hivyo ubaharia ni kazi yenye maisha tofauti, yenye kukabiliana na hatari au majanga mbalimbali ya bahari yanayoweza kupoteza maisha, kufanyakazi na kuishi melini (katika maisha yasiyokimbilika), kujitenga na familia zao, kuwemo safarini kwa muda mefu, kukosa ufungamano na jamii wanazotoka.

Amesema Mabaharia wanachanganyika na watu wenye tamaduni tofauti, kuishi na uwezekano wa kupata maradhi hatari, kufanyakazi ngumu bila kujali wakati, na kukabiliana na vikwazo vya sheria na taratibu za nchi mbalimbali na zile zinazoongoza sekta yenyewe," amesema.

Aidha, amesema Serikali zetu imejipanga vizuri kuhakikisha maslahi ya mabaharia yanalindwa kwa vile imesharidhia Mkataba wa Kimataifa wa Kazi za Baharini wa mwaka 2006 (Maritime Labour Convention 2006) pamoja na kufanya maboresho makubwa katika Sheria za Usafiri Majini za TASAC na ZMA ambazo kwa hakika utakuwa tiba kubwa ya changamoto nyingi zinazowakabili mabaharia wetu hapa Tanzania.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi Dkt.Khalid Salum Mohamed akizungumza katika Maonesho na Maadhimisho ya Siku ya Mabaharia yanayoendelea katika viwanja Shule Njema wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usalama Mazingira Elizabeth MassMassawe akizungumza kuhusiana na Siku ya Maadhimisho Mabahari Duniani ambayo hufanyika Juni 25 yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Nianjema wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkuu wa Mkoa Pwani Abbakari Kunenge akizungumza umuhimu wa Maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani kwa wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo.
Afisa Mkaguzi na Msajili wa Meli wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Gadaff Chambo akizungumza na Wanafunzi wa Wilaya ya Bagamoyo Waliotembelea Banda la TASAC katika maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages