MAMA LISHE MKOANI MBEYA WAISHUKURU KAMPUNI YA ORYX GAS KWA KUTOA ELIMU JUU YA MATUMIZI YA NISHATI YA KUPIKIA. - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, August 27, 2024

MAMA LISHE MKOANI MBEYA WAISHUKURU KAMPUNI YA ORYX GAS KWA KUTOA ELIMU JUU YA MATUMIZI YA NISHATI YA KUPIKIA.

WASHIRIKI mashindano ya kupika kwa gesi ya Oryx wafurahia elimu ya Matumizi sahihi ya ni nishati hiyo huku Kampuni ya Oryx Gas ikisisitiza lengo la mashindano hayo ni kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi kama ambavyo Rais Dk.Samia amedhamiria ifikapo mwaka 2024 asilimia 80 iwe inatumia nishati hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa leo Agosti 27,2024 jijini Mbeya , Meneja Miradi ya Nishati Safi kutoka Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba amesema mashindano hayo yanatija kubwa kwa Mama Lishe na Baba Lishe kwani wanatambua kundi hilo ndilo linaloathirika kiafya kutokana na kutumia kuni na mkaa kwa muda mwingi.

"Mama Lishe anakaa muda mrefu katika anapopika kwa kutumia na mkaa kwani tunaambiwa wananchi wengi wa Tanzania wanafariki kila mwaka kwa kutokana na matatizo ya kupumua au matatizo ambayo yanatokana na madhara ya kuni na mkaa."

"Sasa katika hao watu tunaweza kusema Mama Lishe ndio waathirika wakubwa, kwa hiyo ni jamii ambayo sasa hivi sisi Oryx tunamkakati wa kuhamasisha iachane na kuni na mkaa kwasababu wao wanakaa muda mrefu katika kupika kila siku ndani ya siku 365," amesema Ndomba.

Amesisitiza kwa hiyo Mama Lishe na Baba Lishe wakiamua kubadilika na kuanza kupila kwa nishati safi kutawasaidia kukabiliana na changamoto za kiafya na hivyo kuokoa maisha yao, hivyo mashindano ya kupika kwa gesi ya Oryx kunalenga kuliepusha kundi hilo dhidi ya madhara yanayotokana na kuni na mkaa.

"Lengo la mashindano haya ni katika muendelezo uleule ambao Oryx tumeuanza muda mrefu wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia katika mapishi yake."

"Kwa hiyo ujumbe wetu kwa watu watumie gesi katika kupika mapishi.Tunaamini nishati safi ya kupikia ni suluhisho la changamoto nyingi hasa za kiafya,kimazingira na kiuchumi," amefafanua.

Pia amesema Oryx wanaamini wanalojukumu la kuendelea kuhamasisha nishati safi na ndio maana tumeleta mashindano haya katika eneo la wazi ili kila mtu aone .

Kwa upande wao baadhi ya Mama na Baba Lishe wanaoshiriki mashindano hayo wamempongeza Mbunge wao Dk Tulia Akson pamoja na Oryx Gas kwa KUANDAA mashindano hayo ambayo yanakwenda kuongeza hamasa ya matumizi ya nishati safi katika shughuli zao za kupika.

Akizungumza kuhusu mashindano hayo Mama Lishe Yusra Ismail anayefanya shughuli zake za mama Lishe eneo la Sabasaba jijini Mbeya amesema mashindano hayo yanamanufaa makubwa kwao kwani wanapata elimu kuhusu umuhimu wa kutumia nishati safi lakini na matumizi salama ya nishati hiyo.

"Gesi ya Oryx imekuwa ikitusaidia katika shughuli zetu za mapishi, tunafanya shughuli zetu kwa haraka," amesema huku akieleza kutumia kuni na mkaa kunapoteza muda lakini pia wanaathirika kiafya.

Ameongeza kuwa wanamuunga mkono Rais DK.Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini kwasababu nishati ya gesi ni nzuri na inasaidia katika shughuli zao.

Wakati huo huo Mama Lishe Sabrina Anold anayetokea Kata Ilomba ameseema programu ya nishati safi ya kupikia katika Jiji la Mbeya imekuwa na faida nyingi kwani Mama na Baba Lishe wameendelea kuhamasika kwa kutumia nishati safi ya kupikia katika shughuli zao.

"Dk.Tulia kwa kushirikiana na Oryx Gas wametusaidia sana kwani awali tulikuwa tunatumia kuni na mkaa ambapo tulikuwa tunapoteza muda, kwahiyo baada ya kuja nishati safi tunaweza kutumia muda mzuri na kingine imetusaidia katika eneo la afya kwani wengine macho yamepoteza kuona vizuri kwasababu ya Moshi kwa kutumia kuni."

Wakati huo huo Baba Lishe Yusuph Maumba ambaye ni mshiriki wa shindano la mapishi amesema mashindano hayo yanaongeza hamasa ya kutumia nishati safi ya kupikia na hasa gesi ili kuepuka kuharibu mazingira kwasababu ya kupika kwa kuni na mkaa.

"Kiukweli tutandelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia kwa kutunza mazingira kwa kutumia nishati ya gesi katika kupikia na uzuri chakula kinachopikwa kwa gesi ni kizuri na kitamu . Nimefurahishwa sana na mashindano hayo."

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages