Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Azungumza na Uongozi wa TASAF Ikulu Zanzibar - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, August 27, 2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Azungumza na Uongozi wa TASAF Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 27-8-2024, ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Ndg.Peter Ilomo (kulia kwa Rais) na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ndg. Shedrack Mziray, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 27-8-2024, ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Ndg.Peter Ilomo (kulia kwa Rais) na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ndg. Shedrack Mziray, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ndg.Peter IIomo,baada ya kumaliza mazungomzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 27-8-2024.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza matarajio yake kwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF katika kupambana na umasikini nchini.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo, Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa wa Mfuko huo, Shedrack Salmin Mziray aliefika kujitambulisha kufuatia uteuzi wake hivi karibuni.

Alisema, anatarajia kupitia miradi ya TASAF kwa kaya masikini nchini, itaendelea kuzisaidia kaya zilizo kwenye mazingira magumu zaidi kwa lengo la kuwatoa kwenye umasikini mkubwa sambamba na kutafuta mbinu mbadala kwa kaya zinazoendelea kuwa kwenye umasikini uliokithiri licha ya kupitiwa na miradi ya TASAF.

Rais Dk Mwinyi pia ameupongeza uongozi wa TASSAF kwa jitihada zao za kuinua ustawi wa jamii hasa kwa kuboresha maisha ya familia 22,000 za Zanzibar kupitia mwondelezo wa miradi 15 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.1 vikiwemo vituo vya afya, madarasa, maji safi na salama pamoja na barabara za vijijini.

Pia Rais Dk. Mwinyi alisema, miundombinu hiyo imesaidia kukuza uchumi wa wananchi, kuwaongezea kipato, kwa kuzisaidia kaya masikini kukuza mitaji yao ya biashara na kuwaongezea ajira ndogondogo.

Vilevile Rais Dk. Mwinyi alipongeza mpango wa TASAF awamu ya pili kwa kuendeleza na kusaidia maeneo ambayo serikali zote mbili bado hazijakamilisha.

Naye, Mkurugenzi Mziray alimueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba kwasasa TASAF inatekeleza kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya miradi yake tangu mwaka 2020 hadi kukamilika kwake mwezi Septemba mwaka 2025 ambapo TASAF inatekelezwa na Mamlaka za utekelezaji 187, zikiwemo Halmashauri zote za Tanzania Bara, Unguja na Pemba.

Alisema TASAF inashughulika na asilimia 26 ya kaya masikini nchi nzima na asilimia nane ni kaya masikini zaidi ziliwemo kaya milioni 1.3 wanazozipatia ruzuku kila baada ya miezi miwili na ajira za muda kwa watu wenye uwezo wa kufanyakazi.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa wanazisaidia kaya hizo kuweka vikundi vya maendeleo kwa kuweka na kuwekeza ili kuwaongezea mitaji kwa wastani wa shiingi laki tatu na nusu ili wajiendeleze zaidi.

Alieleza kwasasa TASAF inazishughulikia kaya 394,000 ambazo mradi umezifanyia tathmini na zina mafanikio mkakubwa kati ya hizo kaya 22,000 kutoka Zanzibar ambapo kati yao kaya18,000 zimenufaika na ruzuku za ziada za laki tatu tatu, wanaofanikiwa wanatolewa kwenye mpango kupisha waliokua hawajafanikiwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF, bw. Shedrack Salmin Mziray aliteuliwa kushika wadhifa alionao sasa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan Julai 03 mwaka huu, Kabla ya uteuzi wake bw. Mziray alikuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa TASAF, awali aliikaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF tokea Julai 01 mwaka 2023 baada ya kustaafu kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Ladislaus Joseph Mwamanga hadi alipoteuliwa yeye mwezi mmoja uliopita.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages