RAIS MSTAAFU AWAMU YA SABA AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA MAHAKAMA YA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, December 21, 2024

RAIS MSTAAFU AWAMU YA SABA AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA MAHAKAMA YA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

Rais Mstaafu wa Zanzibar awamu ya saba Dk Ali Mohamed Shein akikunjuwa kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Mahkama ya Mkoa wa Kaskazini hafla iliofanyika kijiji cha Pale Kiongele Wilaya ya Kaskazini A Unguja. Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu "Miaka 61 ya mapinduzi: Amani, Umoja na Mshikamano kwa maendeleo yetu, Mapinduzi Daima."
Rais Mstaafu wa Zanzibar awamu ya saba Dk Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mhandisi Mussa Hamad akitoa maelezo kuhusiana na Jengo katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Mahkama ya Mkoa wa Kaskazini Unguja Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu "Miaka 61 ya mapinduzi: Amani, Umoja na Mshikamano kwa maendeleo yetu, Mapinduzi Daima."
Rais Mstaafu wa Zanzibar awamu ya saba Dk Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mhandisi Mussa Hamad akitoa maelezo kuhusiana na Jengo katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Mahkama ya Mkoa wa Kaskazini Unguja Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu "Miaka 61 ya mapinduzi: Amani, Umoja na Mshikamano kwa maendeleo yetu, Mapinduzi Daima."
Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Mahkama ya Mkoa wa Kaskazini Unguja Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu "Miaka 61 ya mapinduzi: Amani, Umoja na Mshikamano kwa maendeleo yetu, Mapinduzi Daima."
Rais Mstaafu wa Zanzibar awamu ya saba Dk Ali Mohamed Shein akitoa hotuba katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Unguja Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu "Miaka 61 ya mapinduzi: Amani, Umoja na Mshikamano kwa maendeleo yetu, Mapinduzi Daima."
Baadhi ya Majaji na Mahakimu mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Mahkama ya Mkoa wa Kaskazini Unguja Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu "Miaka 61 ya mapinduzi: Amani, Umoja na Mshikamano kwa maendeleo yetu, Mapinduzi Daima."
Rais mstaafu wa awamu ya saba Dr Ali Muhammed Shein amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar iteendelea kujenga majengo ya mahakama Ili kuhakikisha wananchi wanapata haki zao za kisheria.

Ameyasema hayo mara baada ya kufungua jengo la mahakama ya mkoa iliyopo Pale Kiongele mkoa wa kaskazini Unguja ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za maadhimisho ya miaka 61 ya Mapindunzi ya Zanzibar.

Alisema Serikali imekusudia kujenga majengo ya mahakama ili kupunguza mrundikano WA kesi katika mahakama moja Jambo litakalopelekea kesi za wananchi kusikilizwa kwa wakati na kutolewa mamuzi.

Alibainisha kuwa uhaba wa majengo hayo na ufinyu wa nafasi katika majengo yaliyokuwepo siku za nyuma kulipelekea kesi nyingi Kuchelewa kutolewa maamuzi na baadhi ya wananchi kukosa Hali zao kwa kushindwa kufuatilia kesi hizo zilizokuwa zikichukua muda mrefu.

Dk. Shein aliwataka wananchi kuyatumia majengo hayo kudai Haki zao kwa msingi ya Amani na kuwashauri kuwa tayari kutoa ushahidi pale wanapohitajika Ili Haki itendeke wakati WA kutoa maamuzi.

Mbali na hayo aliwaomba majaji na mahakimu kufuata sheria na kutoa haki kwa anaestahiki ili kujenga msingi ya amani ndani ya jamii.

Kwa upande wake mtendaji Mkuu wa mahakama hiyo, Kai Bashir Mbarouk, Alisema serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Dr. Mwinyi imedhamiria kujenga majengo ya mahakama katika mikoa na wilaya za Unguja na Pemba Ili kusogeza Huduma za Sheria karibu na Jamii.

Alibainisha kuwa jengo Hilo la ghorofa moja umezingatia vigezo vya kimahakama na kugharimu zaidi ya bil. 28 fedha za serikali ya Mapindunzi ya Zanzibar na hadi Sasa Zaidi ya shilingi bilioni 14 zimeshalipwa na kueleza kuwa ujenzi umefikia asilimia 83.

Naye Mkuu wa Mkoa wa kasikazini unguja matar Zahoro Masuod aliishukuru Serikali ya awamu ya nane kwa kelekeza miradi mingi ya maendeleo katika mkoa huo ambayo inaendelea kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi katika shamrashamra za sherehe za Miaka 61 ya Mapindunzi ya Zanzibar.

Alisema ni wazi kuwa mapinduzi yamekuja kumkomboa mnyonge kutokana na mateso waliokuwa wakiyapata wakati wa ukoloni na kuleta haki na fursa mbalimbali zilizokosekana katika kipindi hicho.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages