WAZIRI WA UJENZI MAWASILIANO NA UCHUKUZI ZANZIBAR MHE.DK.KHALID SALUM AMEFUNGUA KITUO CHA KUFURAHISHIA WATOTO JAMBIANI MKOA WA KUSINI UNGUJA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, December 21, 2024

WAZIRI WA UJENZI MAWASILIANO NA UCHUKUZI ZANZIBAR MHE.DK.KHALID SALUM AMEFUNGUA KITUO CHA KUFURAHISHIA WATOTO JAMBIANI MKOA WA KUSINI UNGUJA

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk Khalid Salum Mohamed akipunga Mkono kuashiria furaha baada ya kupanda Bembea ya Ndege katika hafla ya Ufunguzi wa Kituo cha Kufurahishia Watoto Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja Ikiwa ni Shamrashamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu-Mapinduzi Daima."

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Salum Mohamed ameitaka jamii kuwalinda na kuwatunza watoto ili kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu na malezi bora.

Ameyasema hayo wakati akifungua Kiwanja cha kufurahishia watoto Paje Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya miaka 61 ya mapinduzi ya Zanzibar,amesema ni vyema kutunza na kuthamini juhudi za Serikali kwa kuwapatia watoto stahiki zao.
Mtoto lazima ashirikishwe katika maamuzi, ahudumiwe katika makuzi yake yawe makuzi bora pia haki ya kupata elimu, haki ya kupata afya pamoja na haki ya kupata burdani na Serikali yetu imejitahidi katika hilo na haya ndio matunda ya Mapinduzi” alisema Dkt. Khalid.

Ameeleza kuwa kuwepo kwa kituo hicho kitaongeza pato la taifa pamoja na kufungua fursa za biashara kwa wananchi katika kujenga mahusiano mema na kuwapa watoto furaha, amani na utulivu.

Dkt. Khalid amesema madhumuni ya Mapinduzi ya January 1964 kuondosha ubaguzi, manyanyaso na mateso kwa wananchi wa Zanzibar na kuwaletea maendeleo na usawa na kuwafanya kuwa huru katika Nchi yao.
Akitoa taarifa ya kitaalamu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Issa Mahfoudh Haji amesema kiwanja hicho kinauwezo wa kubeba watu 3000 kwa wakati mmoja na kitafanyakazi siku za sikukuu na kila mwisho wa wiki.

Amesema kwa mwaka 2024 – 2025 Wiazara imetakiwa kujenga Viwanja vya kufurahishia watoto vitatu katika maeneo tofauti ikiwemo Paje katika Mkoa wa Kusini Unguja ambacho tayari kimezinduliwa vyengine ni Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja na Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amesema ujenzi huo utakamilika kwa muda mfupi kwa kukamilishwa kwa baadhi ya maeneo ikiwemo kuwekwa kwa uzio katika njia ya treni ili kuhakikisha usalama wa watoto pamoja na ujenzi wa bwawa la kuogelea ikiwa ni sehemu ya mafunzo ya kuogelea na kuongeza chachu ya michezo katika eneo hilo pamoja na kuongeza ofisi za utawala.
Zaidi ya Bilioni 1 zimetumika katika ujenzi wa mradi huo wa kiwanja chenye upana wa km 97 na urefu wa km 80 sawa na mita za mraba 7760.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk Khalid Salum Mohamed akikunjuwa Kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi katika hafla ya Ufunguzi wa Kituo cha Kufurahishia Watoto Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu-Mapinduzi Daima."
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk Khalid Salum Mohamed akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Kituo cha Kufurahishia Watoto Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu-Mapinduzi Daima."
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk Khalid Salum Mohamed akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Ayoub Mohamed Mahmoud katika hafla ya Ufunguzi wa Kituo cha Kufurahishia Watoto Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi :Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu-Mapinduzi Daima.
Watoto wakifurahia Pembea ya Gari baada ya kufunguliwa Kituo cha Kufurahishia Watoto Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu-Mapinduzi Daima."
Watoto wakifurahia Pembea ya Gari baada ya kufunguliwa Kituo cha Kufurahishia Watoto Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu-Mapinduzi Daima."

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages