Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Ujenzi wa Jengo jipya la Tume ya Uchaguzi unalenga Kuiimarisha Mifumo ya Kidemokrasia Nchini.
Rais Dk, Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Afisi Kuu ya Tume ya Uchaguzi Maisara, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha Rais Mwinyi ameeleza kuwa Kukamilika kwa Jengo hilo kutamaliźa tatizo Sugu la Muda mrefu lililoikabili Tume ya Uchaguzi (ZEC) la kutokuwa na eneo Bora la kufanyia kazi zake.
Rais Dk.Mwinyi amefahamisha kuwa Uamuzi wa kulifanya Jengo hilo kuwa Kituo kimoja cha Shughuli zote za Uchaguzi (One Stop Centre) kutaongeza Ufanisi kwa Watendaji wa tume.
Halikadhalika, Rais Dk.Mwinyi ameipongeza Tume ya Uchaguzi na Wakala wa Majengo (ZBA) kwa kazi nzuri ya Kusimamia Ujenzi huo kwa Viwango bora na kuihimiza Kampuni ya CRJE ambao ndio Wakandarasi wa Ujenzi huo kumaliza kazi kwa Wakati.
Naye, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ZEC Thabit Idarous Faina ameeleza kuwa Ujenzi huo utakamilika na kuanza kutumika kabla ya Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba Mwaka huu.
Ujenzi wa Majengo Mawili yenye Ghorofa nne Utagharimu kiasi cha Takriban Shilingi Bilioni 11.32 utakapokamilika Fedha zilizotolewa na Mfuko Mkuu wa Serikali, kwa sasa Ujenzi umekamilika kwa Asilimia 81.
Amefafanua kuwa Majengo hayo Mawili moja litatumika kwa Shughuli za Afisi za Tume na jengine kwa ajili ya Huduma za Shughuli za Uchaguzi.
No comments:
Post a Comment