RAIS MWINYI: ONGEZEKO LA WAWEKEZAJI NI UKUAJI WA UCHUMI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Monday, January 6, 2025

demo-image

RAIS MWINYI: ONGEZEKO LA WAWEKEZAJI NI UKUAJI WA UCHUMI

WhatsApp%20Image%202025-01-06%20at%2016.58.40
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa kuna ongezeko kubwa la Wawekezaji katika Sekta ya Utalii hatua inayochangia ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya nchi.

Amebainisha kuwa Ongezeko hilo la Wawekezaji pia linachangia Ongezeko la Watalii wanaotembelea nchini hali inayoimarisha sekta ya Utalii.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipoweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Hoteli ya SSPD-BUHAIRAN iliyopo Bwejuu Mkoa Kusini Unguja Inayomilikiwa na Wawekezaji kutoka Falme za Kiarabu.
Snapinsta.app_472493215_18044152493209140_4862191641631810100_n_1080
Aidha Rais Dk. Mwinyi amefahamisha Kuwa Faida za Utalii ni Kubwa kwa nchi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kuwahimiza Wananchi kuendelea Kuwaunga Mkono Wawekezaji wanaowekeza maeneo mbalimbali.

Amezitaja faida hizo kuwa ni pamoja na fursa za Ajira kwa Vijana zile moja kwa moja na nyengine zisizo za moja kwa moja, Upatikanaji wa soÄ·o kwa bidhaa zinazozalishwa na Wakulima na Wavuvi kwa bidhaa za Baharini na Ongezeko la Pato la Taifa.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amewapongeza Wananchi wa Bwejuu na Mkoa wa Kusini kwa Kuonesha Utayari wao na Kuwakaribisha Wawekezaji hao.
Snapinsta.app_472601233_18044152427209140_1952914311262615340_n_1080
Wakati huohuo Rais Dk Mwinyi ameridhia Ombi lililowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhammed Mahmoud kwa niaba ya Wananchi la kutengenezewa Barabara Ya Kilomita Tatu kwa Kiwango cha lami Kutoka Michamvi Mashariki hadi Michamvi Magharibi.

Ufunguzi wa Mradi huo ni miongoni mwa Shamrashamra za Sherehe za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Snapinsta.app_472608924_18044152397209140_4160479811235441667_n_1080
Snapinsta.app_472467997_18044152490209140_7119701238505650774_n_1080
Snapinsta.app_472836596_18044152475209140_7705760187333174184_n_1080
Snapinsta.app_472806304_18044152466209140_6575942468707674269_n_1080
Snapinsta.app_472541993_18044152511209140_7085049031862366957_n_1080
Snapinsta.app_472697430_18044152454209140_8953654798656237574_n_1080
Snapinsta.app_472622618_18044152436209140_6758096036725718586_n_1080
Snapinsta.app_472592472_18044152502209140_3516782432591662784_n_1080
Snapinsta.app_472427878_18044152415209140_220268537633357090_n_1080
Snapinsta.app_472486716_18044152445209140_867304285585367352_n_1080

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *