WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, January 3, 2025

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI

Watanzania, Wazanzibari na Waumini wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kuendelea kuidumisha amani, utulivu na mshikamano uliopo nchini ili kuweza kuisaidia serikali kuweza kupiga hatua kimaendeleo.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid RIDHAA uliopo MADUNGU WILAYA YA CHAKE CHAKE mara baada ya kumaliza Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Amesema Nchi yoyote ile duniani ili iwe na maendeleo ni lazima kuwepo kwa amani na utulivu kwa wananchi hivyo ni wajibu wa kila muumini,mtanzania na mzanzibari hasa Viongozi wa kisiasa kuendelea kuitunza tunu ya amani iliyopo ambayo imeasisiswa na waasisis wa taifa hili.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ni wajibu wa kila kiongozi wa dini au wakisiasa kuyatumia majukwaa kuhubiri amani ili iendeleee kudumu kwa maslahi mapana ya vizazi vya sasa na baadae.

Alhajj Hemed amewataka wazazi na walezi kukaa pamoja na vijana wao mara kwa mara na kuzungumzia suala la amani pamoja na kuwakataza kutojishuhulisha na mambo yanayosababisha uvunjifu wa amani kwani amani ikitoweka ni vigumu kuirejesha.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapatia elimu zote mbili vijana ili kuweza kupata taifa lenye wasomi na wenyekuitetea dini ya kiislamu kivitendo.

Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Ustadh JUMA HAMADI amewaomba waumini wa Dini ya Kiislam kutumia vyema muda wao katika kufanya ibada kwani Ibada yoyote inahitaji utulivu na ushui ndani yake.

Amesema kuwa kufanya ibada kwa uangalifu kunapelekea kufikia malengo ya ibada hio pamoja na kupata fadhila hapa duniani na kesho akhera.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages