Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrik Ramadhan Soraga (katikati) akikata Utepe kuashiria Uzinduzi wa Barabara za Bumbwini Skuli-Kiongwe 4.30 km hafla iliofanyika Bumbwini Mafufuni Kaskazini Unguja.Ikiwa ni Katika Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye Kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani, Umoja na Mshikamano kwa maendeleo yetu".
Na Rahma Khamis, Unguja
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe, Mudrik Ramadan Soraga amewataka wananchi wa Bumbwini kuzingatia miundombinu iliyowekwa katika barabara ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Aidha amewataka kuacha kujenga karibu na barabara ili kuepusha ajali na kutoa nafasi kwa Serikali kuweka miundombinu nyengine.
Ameyasema hayo Bumbwini Mafufuni Wilaya ya Kaskazini B' katika uzinduzi wa Barabara ya Bumbwini Skuli _ Kiongwe yenye urefu wa km 4.3 ikiwa ni muendelezo wa shamrashamra za kuadhimisha miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Aidha amefahamisha kuwa maendeleo hayana chama kwani dhamira ya Viongozi ni kuhakikisha Zanzibar inakua na maendeleo kwa wananchi wote.
"Tuendelee kumuunga mkono Rais wetu wa Zanznar kwani dhamira yake njema aliokuanayo katika kuimarisha miundombinu" Waziri Soraga.
Ameongezea kuwa Serikali itaendelea kuleta miradi mbalimbali kupitia mawizara ili wananchi wapate maendeleo sambamba na kuipongeza Wizara ya Ujenzi na mawasiliano na Uchukuzi pamoja na Kampuni ya IRIS kwa kubuni miradi mingi na kukamilisha kwa kiwango kinachotakiwa.
"Bumbwini tuliyokua nayo sasa hivi si Ile ya zamani miradi yote imetekelezwa tupewe nini tena wananabumbwini" aliuliza Waziri.
Akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa barabara hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dkt Habiba Hassan amesema mradi wa barabara ya Kiongwe ni sehemu ya mpango wa maendeleo pamoja na mpango mkuu wa usafiri Zanzibar ikiwa ni kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2025.
Ameongeza kuwa miradi yote ya barabara za ndani zimegharimu kiasi Cha Dola za Kimarekani Milioni 80 na laki tatu bila ya ongezeko la thamani ambapo mkataba mwengine umefungwa na Kampuni ya Mawi kutoka Uturuki wenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 79 laki moja 67 elfu 226 kwa ajili ya kugandishia lami ya moto.
Aidha amefahamisha kuwa barabara hiyo inasimamia na Wakala wa Barabara (Zanroad) ambapo muda wa kujengwa kwa kiwango Cha chipsi ni miezi 40 na kiwango Cha lami miezi 30.
Aidha amesema kuwa barabara hiyo ina kiwango Cha ubora na imezingatia vigezo muhimu ikiwemo mabomba yenye vipenye kwa ajili ya huduma za jamii ikiwemo kupitisha Maji na mawasiliano pamoja na michoro ya kugawa usalama kwa watumiaji.
Hata hivyo Katibu ameeleza kuwa barabara hiyo ina uwezo wa kudumu kwa muda wa miaka 10 hadi 20 iwapo itafanyiwa matengenezo kwa muda stahiki.
Nao wananchi wa Wilaya hiyo wamesema kuwa wamefurahishwa kuona barabara hiyo imekamilika kwa kiwango Cha lami kwani wataondokana na adha na usumbufu waliokuwa wakiupata wakati wakiwa safarini.
Ujenzi wa barabara hiyo umeanza Novemba 2023 na kukamilika Novemba 20224 na umegharimu Dola za Kimarekani Milioni mia 2 laki nne 85 mia Tano na 53.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrik Ramadhan Soraga (kulia) akikunjuwa Kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi katika hafla ya Uzinduzi wa Barabara za Bumbwini Skuli-Kiongwe 4.30 km hafla iliofanyika Bumbwini Mafufuni Kaskazini Unguja. Ikiwa ni Katika Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye Kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani, Umoja na Mshikamano kwa maendeleo yetu".
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk Habiba Hassan Omar akitoa Taarifa ya Kitaalamu katika hafla ya Uzinduzi wa Barabara za Bumbwini Skuli-Kiongwe 4.30 km hafla iliofanyika Bumbwini Mafufuni Kaskazini Unguja. Ikiwa ni Katika Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye Kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani, Umoja na Mshikamano kwa maendeleo yetu".
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrik Ramadhan Soraga akitoa hotba ya Uzinduzi wa Barabara za Bumbwini Skuli-Kiongwe 4.30 km hafla iliofanyika Bumbwini Mafufuni Kaskazini Unguja. Ikiwa ni Katika Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye Kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani, Umoja na Mshikamano kwa maendeleo yetu".
Baadhi ya Wananchi mbalimbali na Wafanyakazi waliohudhuria katika hafla ya Uzinduzi wa Barabara za Bumbwini Skuli-Kiongwe 4.30 km hafla iliofanyika Bumbwini Mafufuni Kaskazini Unguja. Ikiwa ni Katika Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye Kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani, Umoja na Mshikamano kwa maendeleo yetu".
Baadhi ya Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya Uzinduzi wa Barabara za Bumbwini Skuli-Kiongwe 4.30 km hafla iliofanyika Bumbwini Mafufuni Kaskazini Unguja. Ikiwa ni Katika Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye Kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani, Umoja na Mshikamano kwa maendeleo yetu".
No comments:
Post a Comment