Mkuu wa Huduma za Rejareja wa
First National Bank, Bw. Francois Botha (Kushoto) na Mkuu wa Matawi na za
Huduma za kibenki, Bw. Kitumari Massawe (Kulia) wakishilia Bango wakati wa
mkutano na waandishi wa habari kama ishara ya kuanzisha huduma ya kutoza
gharama moja kwa miamala ya kibenki kwa wateja wake ambao wana akaunti ya Gold
ya Hundi.
Mkuu wa Matawi na Huduma za
Kibenki, Bw. Kitumari Massawe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam juu ya faida ya akaunti ya Gold ya Hundi ambapo wateja
watalipa shillingi elfu kumi na sita kwa mwezi ambayo ni gharama moja na
kuondoa adha na utaratibu wa kulipa huduma kwa muamala mmoja mmoja.(Kushoto) ni
Mkuu wa Huduma za Rejareja wa Benki hiyo, Bw. Francois Botha na Meneja Masoko
wa First National Bank, Bi. Blandina Mwachang’a (Kulia).
Mkuu wa Huduma za Rejareja wa First National
Bank, Bw. Francois Botha (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es salaam, na kutangaza benki hiyo kuanza kutoza gharama moja kwa miamala
mbalimbali kwa wateja wake ambao wanatumia akaunti ya Gold ya Hundi. (Kushoto )
ni Mkuu wa Matawi na Huduma za kibenki wa First National Bank, Kitumari
Massawe.
First National Bank
Tanzania imetangaza kuanza kutoza gharama moja kwa miamala mbalimbali kwa
wateja wake ambao wana akaunti ya Gold ya hundi ikiwa ni mojawapo ya jitihada
za benki hiyo kuwapa unafuu watumiaji wa huduma za kibenki. Mkuu wa Huduma za
Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha amesema jijini Dar es salaam leo kwamba
benki hiyo itawapatia wateja wake fursa ya kufanya miamala mbalimbali ya huduma
za kibenki mara nyingi wawezavyo kwa gharama moja iliojumuishwa na bila kulipa
gharama za ziada.
“Wateja watalipa shilingi
elfu kumi na sita tu kwa mwezi ambayo ni gharama moja, hii itaondoa adha na
utaratibu wa kulipia huduma kwa muamala mmoja mmoja. Mpango huu unatarajiwa
kuwanufaisha wateja wetu kwa kuwapunguzia gharama za miamala huku wakitumia
fedha hizo kujiongezea akiba zaidi kwenye akaunti zao. Hatua hii ni ya faida
kubwa kwa wateja wetu wa akaunti ya Gold ya hundi na wateja wengine kwa
ujumla”.
Mpango wa gharama moja kwa miamala utajumuisha
utoaji wa fedha kwenye ATM yoyote, miamala ya TigoPesa, malipo ya bidhaa kama
DSTV, LUKU na muda wa maongezi, kuweka maelezo ya kuhamisha fedha toka kwenye
akaunti, kufanya manunuzi ya bidhaa kwa kutumia kadi katika vituo vya mauzo
popote duniani, pamoja na kuweka fedha taslimu na hundi kwenye akaunti ikiwemo
kwenye mpango huu.
No comments:
Post a Comment