Watanzania
wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) pamoja na wanaoishi ndani ya nchi wanatarajia
kufanya mdahalo Aprili 11, 2017 jijini Dar es Salaam, wa kujadili changamoto na
fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini hasa biashara ya viwanda.
Wakati akizungumza
na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ikolo
Investment LTD ambayo ndio muandaaji wa mdahalo huo, Maggid Mjengwa amesema
katika mdahalo huo watajadili maendeleo ya nchi na namna ya kuifanya Tanzania
kuwa na uchumi wa kati unaosukumwa na maendeleo ya viwanda.
“Mdahalo huo
utashirikisha watu wapatao 300 kutoka katika makundi matatu ambayo ni
watanzania wanaoishi na waliokuwa wakiishi ughaibuni na sasa wamerejea nyumbani
pamoja na wanaoishi nyumbani ambao watajadili kufanikisha adhma ya serikali
kuifanya nchi kuwa ya viwanda,” amesema.
Naye Katibu wa
Kongamano hilo, Mwinyi Mwaka Khatib amesema kongamano hilo litasaidia wanaoishi
ughaibuni kupata fursa ya kujadili namna ya kuanzisha viwanda pamoja na jinsi
ya kuboresha bidhaa zinazozalishwa nchini ili zipate soko nje ya nchi.
“Katika harakati za
kutambulisha bidhaa za Tanzania nje ya nchi kuna changamoto sababu
hatujajipanga vizuri kutumia masoko ya nje kutokana na kushindwa kuzalisha
bidhaa toshelezi zenye ubora. Mdahalo huo tutajadili namna ya kukidhi matakwa
ya masoko ya nje ya nchi na kuanzisha viwanda nchini,” amesema.
Khatibu amesema
mdahalo huo umekuja wakati muafaka kutokana kwamba, kwa sasa baadhi ya nchi
zimeanza kutoa fedha za ruzuku kwa diaspora ili waje kuanzisha viwanda kwenye
nchi wanazotoka.
No comments:
Post a Comment