Hatua hii itawawezesha
watanzania wengi zaidi kufikiwa na huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ikiwa
ni sehemu ya kufanikisha azma ya serikali ambayo inazitaka taasisi mbalimbali
za kifedha kuwafikia wananchi na huduma zao hasa kwa maeneo ya vijijini.
Akizungumza wakati wa
uzinduzi huo, mapema leo Aprili 3.2017, Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya
Halotel, Bw. Le Van Dai amesema kuwa ni hatua nyingine kubwa katika utoaji wa
huduma za kifedha kupitia simu za mkononi ambapo sasa huduma ya Halopesa itakuwa
imeunganishwa na benki ya NMB ili kuwawezesha wateja kufanya miamala kwa
urahisi zaidi.
Dai ameendelea kuwa
ushirikiano huo, umeunganisha taasisi kubwa zenye wateja wengi na zilizosambaa
kwa kiasi kikubwa nchini. Tunatarajia huduma hii itapunguza kadhia kwa watumishi
wa taasisi za umma, wakiwemo walimu na watu wa sekta zingine wakiwemo wakulima,
wavuvi na wafanya biashara wanaoishi vijijini ambako huduma za kibenki
hazijafika kote. Maeneo haya kwa kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za
mkononi kuweza kutoa fedha au kuweka kwa njia ya haraka na usalama zaidi.
“Ushirikiano
huu ni wa kipekee katika kurahisisha maisha ya watanzania ambao wamekuwa
wakipata tabu kupata huduma za kifedha kutokana na maeneo wanayoishi. Sisi kama
Halotel hadi sasa tumewafikia watanzania kwa zaidi ya asilimia 95. Hivyo ni
dhahiri kwamba wateja watakaojiunga nasi wataweza kutoa au kuweka fedha huko
huko waliko kupitia kwa mawakala wetu ambao wameenea nchi nzima,” aliongezea Dai.
“Tunatambua
changamoto ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiwasibu Watanzania hasa wa
kipato cha chini. Kwani wengi wao walikuwa wanakwama kuweza kupata huduma za
kifedha kutokana na miundombinu kutowafikia. Mpaka hivi sasa Halotel ina
mawakala zaidi ya 30,000 walioenea nchi nzima. Hii itawawezesha wakazi wa maeneo
ambayo hayakuwahi kuwa na mawasiliano kabisa au huduma za kibenki sasa kuweza
kupata huduma za kifedha kupitia simu zao za mkononi,” alimalizia Naibu
Mkurugenzi wa kampuni hiyo.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu
wa Huduma Binafsi za Kibenki wa NMB, Boma Raballa, amesema ushirikiano huo ni
mafanikio mengine makubwa ya kibiashara kwao hususani katika kupanua wigo wa
huduma zake na namna itakavyoweza kuunganisha teknolojia ili kuwarahisishia
watanzania kupata huduma za kifedha popote walipo.
“Benki
ya NMB ni ya kwanza kutoa huduma za kipekee na zenye ubunifu wa hali ya juu na
tunaamini ushirikiano huu utatuwezesha kuwafikia watanzania wengi zaidi.
Watanzania wanahitaji huduma za kifedha muda wowote na mahali popote walipo.
Hivyo kuja kwa ushirikiano huu kutawaletea uhakika wa kupata fedha tena kwa
njia rahisi kabisa kwa kutumia simu zao za mkononi maana sio muda wote watakuwa
karibu na mashine zetu za kutolea fedha (ATM) au matawi ya benki yetu,” alisema Raballa.
“Kwa kushirikiana na
Halotel tunaamini tutakuwa tumefanikisha lengo la serikali na benki yetu kwa
ujumla katika kuwafikia watanzania wengi zaidi. Hii inamaanisha kuwa wateja wa
kampuni hizi mbili ambazo hawajafikia na huduma aidha za NMB au Halotel basi
watafikiwa kwa pamoja. Mbali na kurahisisha huduma lakini pia itasaidia kwa
kiasi kikubwa kurahisisha kuboresha na kurahisisha hali ya maisha na uchumi kwa
watanzania, yaani kwa watoa na wapokea huduma,” aliongezea Raballa.
Naibu
Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Bw. Le Van Dai akizungumza katika tukio hilo
la huduma ya Halopesa juu ya kuunganishwa na benki ya NMB. Kushoto
ni Henry Mavulla Mwendesha Biashara wa Halopesa na kulia ni Kaimu Mkuu wa
Huduma Binafsi za Kibenki wa NMB, Boma Raballa.
Henry Mavulla Mwendesha Biashara wa Halopesa akizungumza wakati wa tukio
hilo. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Bw. Le Van Dai
Kaimu Mkuu wa Huduma Binafsi za Kibenki wa NMB, Boma Raballa akizungumza
juu ya tukio hilo. kushoto ni Henry Mavulla Mwendesha Biashara wa Halopesa
na katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Bw. Le Van Dai.
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Bw. Le Van Dai akifafanua jambo
wakati tukio hilo
Naibu
Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Bw. Le Van Dai akisaini mikataba wakati wa
tukio hilo. Kulia niKaimu Mkuu wa Huduma Binafsi za Kibenki wa NMB, Boma
Raballa akisaini tukio hilo.
Kaimu Mkuu wa Huduma Binafsi za Kibenki wa NMB, Boma Raballa
akibadilishana nyaraka wakati wa tukio hilo na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni
ya Halotel, Bw. Le Van Dai
No comments:
Post a Comment