Balozi wa Msumbiji nchini Bi Monica Patricio
Clemente akizungumza na viongozi wa TCCIA walioongozana na Makamu wa Rais - Viwanda
Bw. Octavian Mshiu wa kwanza kulia, Mkurugenzi Mtendaji Bw. Gotfrid Muganda
pamoja na viongozi wa TCCIA Mtwara Bw. Swallah S. Swallah Mwenyekiti na Muhidin
Swalehe.
Mkutano huo ulihudhuriwa
na Makamu wa Rais wa TCCIA mwenye dhamana ya Viwanda Bw. Octavian Mshiu
akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Bw. Gotfrid Muganda pamoja na
viongozi wa TCCIA Mkoa wa Mtwara Bw. Swallah S. Swallah ambaye ni Mwenyekiti na
Bw. Muhidin Swalehe - Afisa Mtendaji.
Akizungumza katika
mkutano huo, Makamu wa Rais wa TCCIA - Viwanda Bw. Octavian Mshiu amesema
mapendekezo ambayo TCCIA imewasilisha kwa Balozi wa Msumbiji nchini yanalenga
kutoa ushirikiano wa karibu kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili ambao
utawezesha uanzishwaji wa vituo katika mkoa wa Mtwara ili kurahisisha
upatikanaji wa huduma na misaada ya haraka kwa wafanyabiashara wa pande zote
mbili.
Makamu wa Rais wa TCCIA-Viwanda
Bw. Octavian Mshiu akimkabidhi Balozi Monica Clemente nyaraka maalum baada ya
mkutano na Balozi huyo ofisini kwake mapema wiki iliyopita.
Balozi Bi. Monica
Patricio Clemente amesema amefurahishwa na ugeni alioupata wa uongozi wa TCCIA
na kwamba mapendekezo chanya yaliyoletwa na TCCIA yana nafasi sahihi na muhimu
katika kuboresha ushirikiano wa wafanyabiashara wa Mtwara na Mikoa jirani ya
Msumbiji kwani mahusiano ya aina hiyo yana nafasi kubwa ya kunufaisha jamii ya
wafanyabiashara, kuongeza pato la nchi zote mbili na pia kukuza uchumi wa
maeneo husika.
Balozi Monica ameahidi
kuyafanyia kazi majadiliano na mapendekezo ya TCCIA kwa haraka ili kuongeza
kasi ya ukuaji wa uchumi wa mikoa inayofanya biashara pamoja ambayo matokeo
yake yataleta tija kwa maslahi ya Tanzania na Msumbiji kwa ujumla.
Viongozi wa TCCIA wakiwa katika
picha ya pamoja na watumishi wa ubalozi wa Msumbiji nchini baada ya mkutano wa
Balozi na uongozi wa TCCIA jijini.
Katika mkutano huo
wajumbe kutoka ubalozini humo wamesema moja ya changamoto kubwa inayowakumba
wafanyabiashara wengi ni lugha ambapo wamependekeza pia kuwepo kwa vituo maalum
ambavyo vitakuwa vikitoa elimu ya lugha kwa wafanyabiashara hao ili kuondoa
changamoto hiyo.
Mwenyekiti wa TCCIA
Mtwara Bw. Swallah S. Swallah ameshukuru ubalozi wa Msumbiji kwa ukarimu na
kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya wafanyabiashara wa Cape Delgado
nchini Msumbiji na Mtwara nchini Tanzania.
Pia alieleza juhudi za
Chemba ya Mtwara katika kukabiliana na changamoto ya lugha na kwamba mjini
Mtwara tayari kuna kituo kikubwa cha lugha kinachofundisha watanzania lugha
mbalimbali ikiwemo Kireno ambacho sasa kinatiliwa mkazo zaidi.
Viongozi wa TCCIA wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi
wa ubalozi wa Msumbiji nchini baada ya mkutano wa Balozi na uongozi wa TCCIA
jijini.
No comments:
Post a Comment