WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelitaka
Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), lianze kufanya tathmini ya
kisayansi kuhusu manufaa ya Mifuko yote ya uwekezaji nchini ili kujiridhisha
endapo inawanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa.
Pia amelitaka baraza hilo lifanye
tathmini kuhusu namna ya kuunganisha mifuko hiyo bila ya kuathiri majukumu ya
msingi na mantiki ya kuanzishwa kwake, ili inayofanya kazi zinazofanana
iunganishwe.
Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Aprili
18, 2017) wakati akifungua maonesho ya mifuko ya uwezeshaji katika uwanja wa
Mashujaa mjini Dodoma. Amesema uzinduzi wa maonesho hayo ni fursa nzuri kwa
wananchi kuweza kudadisi kuhusu huduma zitolewazo na Mifuko hiyo na kutoa
ushauri, ili kuboresha huduma.
“Lengo ni kuwa na Mifuko michache,
lakini inayobadilisha maisha ya wanufaika, ambao ni wananchi. Nitafurahi kupata
taarifa hiyo kabla au ifikapo Mwezi Mei, 2018,”
amesema.
Aidha, Waziri Mkuu amesema mapambano
dhidi ya rushwa na ufisadi yanayofanywa na Serikali yanalenga kuwawezesha
Watanzania wengi wafanye shughuli za kujiongezea kipato bila kusumbuliwa na
baadhi ya Watumishi wasio waadilifu.
Ameongeza kuwa “uwezeshaji wananchi kiuchumi ni jambo ambalo
lipo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo
2025; Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2017 – 2020/2021,”.
Amesema kuwawezesha wananchi kiuchumi,
sio ubaguzi wala upendeleo, bali ni jitihada za makusudi za kuwashirikisha
wananchi walio wengi ambao kwa sababu za kihistoria, wamejikuta wakiwa nje ya
mfumo rasmi wa kiuchumi, hivyo kubaki kwenye hali duni jambo ambalo ni hatari
kwa ustawi na usalama wa nchi.
Waziri Mkuu amesema jitihada za
uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizoanza tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza na
kuendelezwa na awamu zote zilizofuata, ambapo kwa sasa kuna mifuko 19 ya
kuwezesha wananchi kiuchumi.
Amesema mifuko hiyo imesaidia
upatikanaji wa mitaji kwa wajasiriamali na kupunguza kiwango cha umaskini
nchini. “Hadi kufikia mwaka 2016 Mifuko hiyo kwa
pamoja ilikuwa imetoa mikopo yenye thamani ya sh. trilioni 1.759 kwa
wajasiriamali 400,000.
Awali Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi.
Beng` Issa alisema maonesho hayo ya siku nne yatawezesha kuwaongezea wananchi
uelewa juu ya shughuli zinazofanywa na mifuko ya uwezeshaji.
Amesema kati ya mifuko 19 ya uwezeshaji
mifuko 13 imeweza kushiriki katika maonesho hayo ya kwanza kufanyika nchini,
ambapo kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Wezesha
wananchi kiuchumi ili kujenga uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda”
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank
PLC, Bw. Sabasaba Moshingi aliyezungumza kwa niaba ya washiriki alisema
madhumuni ya maonesho hayo ni kukuza uelewa juu ya uwepo wa mifuko ya kuwezesha
wananchi kiuchumi na fursa zitolewazo na mifuko hiyo.
Pia kuhamasisha wananchi juu ya
kujijengea utamaduni wa kujiwekea akiba na kuwekeza katika miradi yenye kuleta
faida pamoja na uanzishwaji na uimarishwaji wa vikundi na miradi ya kiuchumi
ili kuunganisha wananchi na fursa za huduma ya mikopo, mafunzo na huduma
nyingine zinazotolewa na mifuko hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi
wa manispaa ya Dodoma, Bw. Godwin Kunambi (wapili kushoto) hundi ya Shilingi 1,
469, 358,0 00/= kwa ajili ya vijana kabla ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya
Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa mashujaa mjini Dodoma Aprili
18, 2017. Wanne kushoto ni Wziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Naibu Wziri
wake, Anthony Mavunde. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini , Christina
Mndeme na watatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,
Beng Issa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Kitengo
cha Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya TPB, Noves Moses (kulia) na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi (wapili kulia) cheti maalum cha
kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya
kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017.
Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mzee
Maarufu wa Dodoma, Job Lusinde baada ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya
Uwezeshaji Wananchi ya serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili
18, 2017. Wengine pichani kutoka kulia ni Waziri wan chi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, AjiraKazi, Jijana, ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme na Katibu Mtendaji wa Baraza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng Issa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TBP, Bw. Sabasaba
Moshingi akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Mifuko ya Uwezeshaji ya Serikali
katika maonyesho ya mifuko hiyo yaliyozinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwasalimia wananchi
wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofungua Maonyesho ya Mifuko ya
Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Uhuru mjini Dodoma Aprili 18,
2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika maonyesho ya Mifuko ya
Uwezesha Wananchi ya serikali baada ya kufungua maonyesho hayo kwenye Uwanja wa
Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa
Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya TPB, Noves Moses (kulia) na
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi (wapili kulia) cheti
maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali
kabla ya kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18,
2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa
Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya TPB, Noves Moses (kulia) na
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi (wapili kulia) cheti
maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali
kabla ya kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18,
2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati
alipofungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye
uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Meneja wa
PPF wa Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian cheti maalumu cha
kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya
kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikilza Bi. Evelyne
Mandenje amabaye ni mmoja wa wajasiriamali walionufaika na mikopo inayotolewa
na Benki ya TIB wakati alipotembelea banda la wasindikaji vyakula kabla ya
kufungua Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja
wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na
watumishi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakati alipotembelea banda la benki
hiyo kwenye maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali
aliyoyafungua kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista
Mhagama wakijadili jambo katika maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya
Serikali yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma
Aprili 28, 2017. Kulia ni Afisa Mwandamizi wa Fedha wa Benki ya TIB, Kenneth
Lusesa.
No comments:
Post a Comment