Tuesday, April 18, 2017

HAWA NDIO MARAIS WALIOCHAGULIWA WAKIWA NA UMRI MDOGO ZAIDI DUNIANI
Katiba za nchi mbalimbali zimeweka wazi umri unaofaa
kwa mtu kugombea nafasi ya uongozi hasa Rais ingawa kiwango hicho hutofautiana
kulingana na nchi;
Kwa mfano, Tanzania mgombea wa Urais lazima aanzie
miaka 40 na kuendelea. Zipo pia nchi nyingine ambazo kigezo cha umri sio muhimu
sana kumfanya mtu agombee nafasi hiyo na wakati mwingine nafasi hiyo hurithiwa
Leo napenda kuwaletea listi ya Marais waliowahi
kuchaguliwa wakiwa na umri mdogo duniani hadi kufikia 2017 ambapo Rais wa sasa
wa Korea Kaskazini ‘Kim Jong Un’ akiwa ndiye Rais mdogo zaidi kuwahi kuchaguliwa.
1: Kim Jong Un
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anashikilia
rekodi ya kuwa Rais mdogo zaidi kuwahi kuchaguliwa duniani ambapo aliingia
madarakani akiwa na umri wa miaka 26 mwaka 2011 akirithi kiti cha baba yake Kim
Jong Il. Sasa Rais Kim Jong Un ana umri wa miaka 33.
2: Tamim Bin Hamad
Ni Rais wa Qatar ambaye aliteuliwa kushika wadhifa
huo mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 30. Tamim Bin Hamad ana umri wa miaka 35
kwa sasa akikamata nafasi ya pili kuwa Rais mwenye umri mdogo zaidi duniani.
3: Jigme khesar
Huyu ni Mfalme wa Bhutan, nchi ndogo katika Bara la
Asia inayopakana na China na India. Mfalme wa nchi hii ndiye kiongozi mdogo
zaidi kuwahi kuteuliwa wakati anaanza uongozi wake. Jigme khesar aliteuliwa
kuwa Mfalme wa nchi hiyo akiwa na umri wa miaka 25 mwaka 2006. Sasa ana umri wa
miaka 37.
4: Atifete Jahjaga
Atifete Jahjaga anashikilia rekodi ya kuwa Rais
mdogo mwanamke kuwahi kuchaguliwa duniani. Jahjaga alikuwa Rais wa Kosovo
kuanzia April 2011 akiwa na umri wa miaka 35 na kumaliza muda wake mwaka 2016
akiwa na umri wa miaka 40.
5: Andrzej Sebastian Duda
Andrzej Duda ni Rais wa sita wa Poland ambaye
alichaguliwa mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 42. Kabla ya kuwa Rais wa nchini
alikuwa Mbunge wa Bunge la Ulaya.
6: Joseph Kabila
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph
Kabila alichaguliwa mwaka 2001 siku kumi baada ya kifo cha baba yake Laurent
Kabila wakati huo akiwa na umri wa miaka 28. Joseph Kabila ana umri wa miaka 45
kwa sasa.
Tags
# SKONGA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
NEEC FANYENI TATHMINI YA KISAYANSI KUHUSU MANUFAA YA MIFUKO YOTE YA UWEZESHAJI-MAJALIWA
Older Article
WLAC WAANZISHA MABONANZA KUHAMASISHA JAMII KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA
Upatu: Mbinu yakujikwamua yenye tamu na chungu
Hassani MakeroJan 27, 2025FEZA Boys yatikisa ufahulu wa wanafunzi kidato cha nne
Hassani MakeroJan 23, 2025TIBA YA KWELI YA UGONJWA WA KIFUA KIKUU (TB)
Hassani MakeroNov 10, 2024
Labels:
SKONGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment