Wanafunzi wa kijiji cha “Ronjo Umasaini” Kata ya Duga Maforoni, Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga wanasomea ndani ya Kanisa kutokana na kijiji hicho kukosa shule.
Mchungaji wa kanisa
hilo, Clement amesema wamelazimika kutoa Kanisa hilo ili watoto wasikose elimu
ambayo itakuja kuwa msaada katika maisha yao ya baadae.
Mwalimu wa Darasa
Magreth Lishule amesema wanalazimika kuwasomesha wanafunzi 105 chumba kimoja
kuanzia darasa la awali hadi la tatu na wakimaliza ndio ukomo wa elimu yao.
Alisema uwezo wa walimu ambao yeye na mwenzake wamejitolea; wamekuwa wakifundisha hadi darasa la tatu na kutokuwa na uwezo wa kufundisha madarasa ya juu.
Mwalimu
wa darasa Magreth Lishule akiangalia kazi za mmoja wa wanafunzi wake darasani.
No comments:
Post a Comment