Baadhi ya watu wamekuwa
wanachukulia kirahisi
ulaji wa matunda, lakini unapaswa kujua kwamba matunda ni muhimu kwa afya zetu
kwani yanatukinga na magonjwa mbali mbali na pia hutengeneza muonekano mzuri wa
ngozi ya miili yetu.
Kunakila sababu za
kukubali kuwa matunda ni muhimu sana kwa afya zetu kwa sababu huongeza vitamin
kibao; zifuatazo ni sababu zinazokufanya ule matunda kila siku:
AVOCADO: Tunda
hili limekuwa maarufu sana kwa kutengenezewa juice, lakini huenda watu wakawa
hawalipendi kwasababu ya kutokuwa na sukari katika radha yake. Tunda hili
linavitamini kibao, ambapo pia huongeza mafuta mwilini, kwa wale walitumialo
mara kwa mara.Unashauriwa kula au kunywa juice ya avocado wakati wowote endapo
kama huna matatizo yoyote yanayohusiana na kuzidi kwa mafuta mwilini.Pia tunda
hili huongeza uzito endapo utalitumia mara kwa mara.
APPLE: Hili
ni tunda maarufu sana duniani lihusishwalo na wapendanao, lakini tunda hili
pamoja na kupewa umaarufu mkubwa duniani na kuwa na vitamini na madini kibao,
pia lina kazi kubwa sana katika kukupa muonekano mzuri wa ngozi ya mwili
wako.Tunda hili husaidia kuboresha mzunguko wa damu mwilini pamoja na kuhifadhi
ngozi isipoteze uhalisia wake.
NDIZI: Hili
pia ni tunda lenyejina kubwa kwa watu wengi wanaojali ulaji wa matunda, kwani
nitamu na lenye ladha safi.Tunda hili husaidia kulainisha ngozi ya uso
iliyokauka, kwa mfano utakuta kuna baadhi ya mafuta au losheni zimecholwa
ndizi.Kula ndizi ili urekebishe ngozi ya uso wako pamoja na kuupa uwezo mzuri
wa ukumeng'enya chakula.
PAPAI: Ni
tunda sahihi kabisa katika kukupa ngozi yenye mafuta, kurudishia au kuziba
sehemu zilizoumia na kunyofoka katika ngozi yako. Papai pia
hunga'arisha rangi ya ngozi yako, yote haya hufanyika na enzyme inayotokana
papai ambayo huitwa papain. Endapo kama unataka kutumia papai katika ngozi yako
ya uso, basi chukua asali changanya na papai lililo iva na paka usoni kwako kwa
dakika 10 kisha safisha, kisha utaona kitakachotokea katika uso wako,
utaonekana kama ngozi ya mtoto wa siku mbili.
CHUNGWA:
Hili ni chungwa maarufu sana linalosaidia kurudishia ngozi iliyodhurika na
kuupa uhalisia wa ngozi yako. Jinsi ya kutumia ni rahisi sana, chukua juisi ya
chungwa ya baridi kisha paka usoni, acha kwa dakika 10 kisha osha utaona
matokeo yake.
Baadhi ya watu wamekuwa
wanachukulia kirahisi
ulaji wa matunda, lakini unapaswa kujua kwamba matunda ni muhimu kwa afya zetu
kwani yanatukinga na magonjwa mbali mbali na pia hutengeneza muonekano mzuri wa
ngozi ya miili yetu.
Kuna kila sababu za
kukubali kuwa matunda ni muhimu sana kwa afya zetu kwa sababu huongeza vitamini
kibao; zifuatazo ni sababu zinazokufanya ule matunda kila siku.
No comments:
Post a Comment