Mwigizaji Clifton James,
aliyeigiza kama Liwali JW Pepper kwenye filamu mbili za James Bond, amefariki
dunia akiwa na miaka 96.
Alifariki
karibu na mji wake aliokulia wa Gladstone, Oregon, siku ya Jumamosi kutokana na
matatizo ya ugonjwa wa kisukari.
James
alizaliwa mwaka1920 akiwa ni mtoto wa kwanza Bi Grace na Bw Harry James na kufariki tarehe 16 April 2017.
James
alifahamika sana kutokana na uigizaji wake pamoja na Sir Roger Moore katika
filamu za Bonds za Live and Let Die na The Man with the Golden Gun
miaka ya sabini.
Binti
yake Lynn amesema: ''Alikuwa mtu mpenda watu na mwenye uwazi sana. Alipendwa
sana na kila mtu.''
Aliongeza:
"Sidhani alikuwa na adui hata mmoja. Kwa kweli tulibarikiwa kuwa na yeye
maishani."
No comments:
Post a Comment