Mwenyekiti
wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Dkt. Omary Chillo (kulia) akifafanua jambo
kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya mbio za
heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza
magonjwa yasiyoambukizika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni
Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Lucas Nkungu na kushoto
ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit
Bi. Rebecca John.
Katibu
Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John (katikati)
akisisitiza jambo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea
maandalizi ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la
kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika mapema hii leo jijini
Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi.
Ombeni Zavara na kulia ni Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa
Dar es Salaam
Bw. Lucas Nkungu.
Katibu
Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi. Ombeni Zavara akizungumza na
wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ya mbio za heart marathon na upimaji
wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika
mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya
Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John.
Taasisi ya Tanzania Health Summit yaandaa mbio
za nusu Marathon na Upimaji wa afya kwa lengo la kusaidia juhudi za serikali
katika kupunguza magonjwa yasioambukiza, mbio hizo zinazotarajia kufanyika
Aprili 26 katika barabara ya Kaole iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Taasisi
hiyo Rebecca John wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki.
“Kamati ya maandalizi ya
ya mbio za Heart Marathon inapenda kuwa taarifu wadau wote wa sekta ya afya
hapa nchini na jamii kwa ujumla juu ya mbio za Heart Marathon na upimaji wa
afya ili kuungana na serikali katika juhudi za kupunguza magonjwa
yasiyoambukiza” alisema Rebecca.
Aliongeza kuwa kwa mwaka huu mbio hizi
zitashirikisha washiriki zaidi ya elfu mbili kutoka rika mbalimbali wakiwemo
vijana, watoto, wazee, makundi ya watu wenye ulemavu na watu wenye magonjwa
yasiyoambukiza.
Pia washiriki watapata nafasi ya kupima afya
magonjwa mbalimbali kama vile shinikizo la damu, wingi wa sukari katika damu,
kiasi cha mafuta mwilini, uchunguzi wa uvimbe katika matiti na kupata ushauri
wa wataalam kuhusiana na vyakula bora, magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
Aidha Bi. Rebecca aliongeza kuwa washiriki
watakimbia umbali tofauti, kwani kuna mbio ndefu za kilometa 21.1 kwa ajili ya
wakimbiaji wazoefu, kilometa 10 kwa wakimbiaji wa kati, kilometa 5 kwa
wakimbiaji wa kawaida, kifamilia na kampuni na mbio za watoto chini ya miaka 12
ni meta 700 na zawadi itatolewa kwa mshindi wa kilometa 21.1 pekee kwa kiasi
cha shilingi laki tano.
Kwa upande wake Rais wa Tanzania Health Summit
Dr.Omary Chillo alisema kuwa washiriki watatakiwa kutoa kiasi kidogo cha fedha
kwa ajili ya kununua flana pamoja na kifaaa maalum cha kuhesabia muda wakati wa
kukimbia ila maji ya kutosha yatatolewa bure kwa ajili ya wakimbiaji.
Aliongeza kuwa wameimarisha ulinzi kwa kushirikiana na jeshi la polisi na ili kulinda usalama kwa washiriki na wananchi watakaokuwepo katika mashindano hayo.
“Wananchi wasiwe na wasiwasi
wa usalama kwani tutashirikiana na jeshi la polisi ili kuimarisha usalama na
tumeweza kupata baraka nyingi kutoka kwao kwa kuweza kushirikiana nao” aliongeza Chillo.
Pia Katibu msaidizi wa Chama cha Riadha nchini
Bi Ombeni Zavala alisema anashukuru wananchi wanavyoweza kujitokeza katika
mashindano hayo na pia anawaomba wananchi hasa vijana waendelee kujitokeza kwa
wingi kwani wanaweza kupata nafasi ya kuunda timu ya Taifa ya vijana chini ya
miaka 17.
Naye Sajenti Isaya Mlokozi kutoka kanda ya usalama
barabarani alisema jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani litahusika
vizuri katika sehemu inayowahusu kuhakikisha watu wanafanya zoezi hilo kwa hali
ya usalama na litajumuika na wananchi popote pale watakapokuwa wanakwenda.
Mashindano haya mwaka jana yalifanyika katika
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam lakini kutokana na kuongezeka kwa watu mwaka huu
yatafanyikia barabara ya Kaole yenye kauli mbiu ‘Piga hatua moja mbele ya
magonjwa Sugu’
No comments:
Post a Comment