Kaimu
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto, Edward Mbanga (katikati), akizindua Mpango wa Bima ya Afya kwa
Gharama Nafuu katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke,
Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zurich Insurance
Blockers, Sudi Simba na Rogation Selengia ambaye ni Mkuu wa Uendeshaji wa Idara
ya Tiba ya Kampuni ya Jubilee Insurance. Kampuni hizo mbili zitashirikiana
kuuendesha mpango huo utakaofadisha familia ya watu wanne kwa kulipa
Sh.
174,000 kwa mwaka.
Kaimu
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto, Edward Mbanga akizindua Mpango wa Bima ya Afya kwa Gharama Nafuu
katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es
Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto, Edward Mbanga akizungumza na vyombo vya habari kuhusu manufaa
ya bima hiyo wakati akizindua Mpango wa Bima ya Afya kwa Gharama Nafuu katika
hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam.
Mkuu wa
Uendeshaji wa Idara ya Tiba ya Kampuni ya Jubilee Insurance, Rogation Selengia
akimkabidhi zawadi ya fulana Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zurich Insurance Blockers, Sudi Simba (kushoto)
akimkabidhi zawadi ya fulana Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga wakati wa
uzinduzi wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Gharama Nafuu 'Afya Wote' katika hafla
iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam. Kampuni
hiyo na Jubilee Insurance zitashirikiana kuuendesha mpango huo utakaofadisha
familia ya watu wanne kwa kulipa Sh. 174,000 kwa mwaka.
Nembo ya
mpango huo ambao wanachama wake watanufaika kwa kuhudumia katika hospitali
zaidi ya 200 nchini.
Mkuu
wa Idara ya Tiba wa Kampuni ya Jubilee Insurance, Keneth Agunda, akielezea kuwa
watakaonufaika katika mpango huo ni baba, mama na watoto wawili na endapo
familia itataka kuongeza idadi basi kila atakayeongezwa atatozwa sh. 100,000
kwa mwaka.
Kaimu
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto, Edward Mbanga akifafanua kuwa kwa hivi sasa ni asilimia 25 ya
wananchi ndiyo waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hivyo serikali
inawakaribisha watu binafsi kuanzisha bima za afya kama kampuni hizo mbili
zilivyofanya.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zurich Insurance Blockers, Sudi Simba akiwaelezea
wananchi faida mbalimbali watakazopata kupitia bima hiyo ya gharama
nafuu.Alitaja huduma zitakazokuwa zinatolewa kuwa ni; magonjwa sugu, huduma za
kulazwa, magonjwa ya nje, kulazwa kwa majeraha ya macho-ajali, meno, uzazi wa
kujifungua kawaida na upasuaji na ubani wa mazishi kwa kila mwanachama sh.
500,000.
Wananchi
wakisikiliza kwa makini wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya
maofisa wa kampuni hizo.
Malkia wa
Mipasho, Khadija Kopa akiongoza kuimba wimbo wa kampeni ya kuhamasisha kujiunga
na bima hiyo.
Akina
mama wakitafakari kuhusu mpango huo wa Bima.
No comments:
Post a Comment