Hatua hii inatokana na
marufuku iliyowekwa na serikali ya Rais Donald Trump kuzuia baadhi ya raia wa
mataifa yenye Waislamu wengi kuzuru Marekani, pamoja na masharti mengine makali
ya kiusalama.
Shirika hilo la ndege la
Dubai limesema mabadiliko hayo yanatokana na kushuka kwa idadi ya watu
wanaosafiri kwenda Marekani.
Mwezi Machi, Marekani
ilipiga marufuku vifaa vya kielektroniki ambavyo ni vikubwa kuliko simu za
rununu visibwebwe kwenye sehemu ya mizigo ya ndege kutoka viwanja 10 vya ndege.
Viwanja hivyo ni pamoja
na vya Dubai, na mataifa mengine ya Mashariki ya Kati, Afrika kaskazini na
Uturuki.
Rais Trump pia alitia
saini amri ya kuwazuia wahamiaji na raia kutoka mataifa kadha yenye Waislamu
wengi kutoka Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika wasizuru Marekani.
Tayari kuna kesi
zilizowasilishwa mahakamani kupinga marufuku hizo.
Msemaji wa Emirates
alisema: "Hatua za karibuni zilizochukuliwa na serikali ya Marekani
kuhusiana na kutolewa kwa viza za kuingia nchini humo, masharti makali ya
ukaguzi wa kiusalama na vizuizi kuhusu vifaa vya kielektroniki kwenye mizigo ya
ndege vimeathiri moja kwa moja nia ya wateja kutaka kusafiri kwa ndege kwenda
Marekani.
"Kwa miezi mitatu
iliyopita, tumeshuhudia kushuka pakubwa kwa idadi ya wateja wanaowasilisha
maombi ya kutaka kutumia ndege zetu kuingia Marekani."
Rais wa Emirates Tim
Clark alisema mwezi jana kwamba idadi ya watu wanaotaka kwenda Marekani
imeshuka kwa theluthi moja tangu kutolewa kwa tangazo la Bw Trump.
Emirates imesema
itapunguza safari za ndege kwenda Fort Lauderdale na Orlando kuwa tano kila
wiki kuanzia mwezi Mei, badala ya safari moja kila siku.
Aidha, itapunguza safari
kutoka mbili kila siku kwenda Seattle na Boston hadi moja kila siku mwezi Juni,
na kwenda Los Angeles kwa kiwango sawa Julai.
Washindani wa Emirates,
Etihad kutoka Abu Dhabi hata hivyo wanasema hawajashuhudia kupungua kwa watu
wanaotaka kutumia ndege hizo kwenda Marekani wiki za karibuni.
No comments:
Post a Comment